Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi, (NEC), Beng’ Issa, (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Benjki ya Posta,
Sabasaba Moshingi, (wapilia kulia), Rais wa VICOBA Endelevu Tanzania, Devota
Likokola, (wapili kushoto), Mwanasheria wa Benki ya Posta Tanzania, Mystica
Mapunda Ngongi, (wakwanza kulia), wakiwa wameshikana mikono baada ya benki hiyo
kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano kati ya baraza na benki hiyo, katika
kuwawezwesha wana VICOBA kiuchumi. Hafla hiyo ilifanyika leo Julai 14, 2015. kwenye ukumbi wa
wizara ya fedha jijin I Dar es Salaam.
BARAZA
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NDC), na Benki ya Posta Tanzania,
(TPB), wamesaini makubaliano ya ushirikiano wa kuwawezesha wanachama wa VCOBA
nchini.
Akizungumza
wakati wa hafla ya kutiliana saini makubaliano nhayo kwenye ukumbi wa wizara ya
fedha jijini Dar es Salaam leo Julai 14, 2015, Katib u Mtendaji wa baraza hilo, Beng’ Issa,
alisema, Katika juhudi za kuwawezesha watanzania kiuchumi kupitia upatikanaji
wa mitaji na kuendeleza ujasirimali nchini, Serikali kupitia Sheria ya Taifa ya
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004, ibara ya IV, sehemu ya 16 iliagiza
uanzishwaji wa Mfuko wa Taifa wa Uwezeshaji Mwanachi yaani ‘’Mwananchi
Empowerment Fund,”.
“Katika
kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa mitaji yenye gharama nafuu kwa
wajasiriamali nchini, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi limesaini
hati za makubaliano na Benki ya Posta Tanzania katika kusimamia udhamini wa
mikopo yenye masharti nafuu kwa
makundi mbali mbali ya wajasiriamali nchini yanayokidhi masharti
husika.” Alisema Beng’i.
Mfuko
huu utakao simamiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ni pamoja
na kutoa fursa kwa wananchi katika makundi au mtu mmoja mmoja kupata mitaji ya
kuwekeza kwenye miradi ya kiuchumi kupitia mikopo ya moja kwa moja au udhamini
(direct lending or guarantee system).
Ili
kutimiza azama hiyo baraza limeamua kushirikiana na benki ya ;posta Tanzania
ambayo ina mtandao mpana, kutekeleza azma hiyo ambapo wananchama wa VICOBA,
watapata mikopo na mafunzo kutoka benki ya posata.
Kwa
aupande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi,
alisema, benki yake ni benki ya wananchi
na hivyo unayo furaha kubwa kushirikiana na NE, ili kuwakwamua wananchi
kiuchumi kwa kupata mikopo itakayowazsaidia kuendesha shughuli zao za kiuchumi.
“Benki
ya Posta inayo furaha kubwa kushirikiana na Baraza hili ili kuwawezesha
wananchi wengi zaidi kupata huduma za kifedha kwa gharama nafuu kupitia mpango
huu.” Alifafanua Moshingi.
Alisema,
Benki ya Posta inaamini kuwa hii ni fursa muhimu kwa vikundi hivi visivyo
rasmi kufungua akaunti na kuweka fedha
zao mahala salama. Hili litawawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi zaidi,
na hatimaye wataweza kupatiwa mikopo nafuu kwa ajili ya kukuza biashara zao.
Hadi sasa Benki imefungua zaidi ya akaunti 340 za vikundi. Vikundi hivi
vitafaidika pia na huduma ya TPB POPOTE, itakayo wawezesha kupata huduma za
kifedha popote pale walipo.
Katibu Mtendaji wa NDC, Beng'i Issa
Mkurugenzi Mtendajin wa TPB. Sabasaba Moshingi
Moshingi, (kulia), Beng'i(katikati) na Lokokola, wakibadilishana mawazo mwishoni mwa hafla hiyo
Devota akishukuru Mungu, baada ya kufikiwa makubaliano hayo ambapo wanachama wake ni wafaidika wakubwa
Picha ya pamoja, Viongozi wa TPB, NDC, na Vicoba endelevu, wakiwa katika picha ya pamoja na waliohudhuria hafla hiyo
No comments:
Post a Comment