MD Digital

Saturday, July 18, 2015

AMON MPANJU ARUDISHA FORM YA KUMKABILI HALIMA MDEE JIMBO LA KAWE

Ikiwa zoezi la uchukuaji na urejeshwaji wa form za kuomba ridhaa ya vyama mbalimbali kuwania nafasi ya ubunge na udiwani linazidi kushika kasi naye aliyekuwa mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu nchini Tanzania AMON MPANJU amejitosa katika kinyanganyiro hicho kuwania nafasi ya ubunge ndani ya jimbo la kawe jijini Dar es salaam.


Aliyekuwa mjumbe katika bunge maalum la katiba Tanzania ambaye ni mlemavu wa kuona  AMON MPANJU leo akikabidhi form kwa katibu wa ccm wilaya ya kinondoni bwana ATHMAN SALUM SHESHA mapema leo.
Mapema leo katika ofisi za makao makuu ya ccm kinondoni Bwana MPANJU alirejesha form ya kuwania ubunge katika jimbo la kawe ambapo akizungumza na wanahabari baada ya kurejesha form hiyo alisema kuwa lengo la kutaka kuwa mbunge wa jimbo la kawe ni kutokana na dhamira ya dhati aliyonayo ya kutumia taaluma yake ya uanasheria katika kuwasaidia watanzania hasa waishio katika jimbo la kawe.
AMON MPANJU hapa akisaidiwa na mpambe wake kutia saini katika form zake kabla ya kuzikabidhi rasmi

AMON MPANJU ambaye nyote yake ilingara wakati aliupopata nafasi ya kuwakilisha katika bunge maalum la katiba wakati wa uundwaji wa katiba mpya amesema kuwa lazima watanzania watambue mchango wa watu wenye ulemavu kama yeye na walemavu wengine na kuwapa nafasi katika maswala ya uongozi kwani walemavu ni watu makini na wanaweza kushiriki katika maswala mbalimbali ya kulijenga taifa.

AMON MPANJU akizngumza na wanahabari mbalimbali waliofika kushughudia akirejesha form leo
Ameongeza kuwa sasa ni wakati wa watanzania kuacha kuchagua mtu kwa kufwata mkondo na badala yake ni muda muafaka wa watanzania kuchaguz viongozi ambao watawasaidia katika kuwaletea maendeleo huku akijinasibu kuwa yeye ni mmoja wao.

Amesema kuwa wananchi wa kawe wakimpa nafasi yeye kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha kuwa maswala yote yanayohusu maamuzi ya wanakawe dhana ya ushirikishwa wa wananchi wote itatumika ili kila mwana kawe anufaike na rasilimali zake.

Aidha katika hatua ninyine AMON MPANJU amewaomba watanzania hususani wanakawe kuhakikisha kuwa wanajitokeza kwa woingi katika uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura zoezi ambalo linataraji kuanza siku terehe 22 mwezi huu katika mkoa wa Dar es salaam ili waweze kuwa na fursa ya kuchaguz viongozi wanaowataka.

Mwanaharakati huyo akiondoka katika ofisi za CCM kinondoni baada ya kumaliza zoezi la urejeshaji wa form

AMON MPANJU anajitosa katika jimbo la kawe huku kukiwa na upinzani mkubwa wa wana ccm  zaidi ya 20 ambao nao wanawania ubunge katika jimbo la kawe huku upande wa upinzani ikiwa bado upinzani mkubwa ni kutoka kwa mbunge wa sasa wa jimbo hilo HALIMA MDEE kutoka CHADEMA.

No comments: