MD Digital

Saturday, August 29, 2015

BUNGE LA WATOTO OYSTERBAY SHULE YA MSINGI MKOANI MANYARA WAFANIKIWA KUWARUDISHA WATOTO WA MITAANI SHULE


Abdallah Waziri - ambaye ni mmoja wa watoto wa mitaani aliyerudishwa shule kwenye kikao cha leo.
Abdallah Waziri, Asia Mtibua na Mwalimu Gaudensia Igoshalimo wakimkaribisha Abdallah Waziri shuleni.
Mmoja wa wajumbe akitoa maoni yake katika kikao  cha bunge katika shule ya oysterbay mkoani manyara
Mbunge Nasri Selemani akifuatilia hoja kwa makini.wakati kikao cha bunge la watoto likiendelea katika shule ya oysterbay mkoani manyara 

 Mbunge Nasri Selemani ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa nyumbani na sasa kwa jitihada za bunge amerudishwa shuleni,,akichangia hoja.
Mtangazaji wa Kipindi cha Tafakari Time Benedicta Mrema akizungumza na Abdallah Waziri na kumkabidhi mchango wa shilingi 57,800 aliochangiwa kwa ajili ya kumuwezesha mahitaji ya shule.

Raisi wa Bunge la watoto Oysterbay, Manyara - Sarah David akitoa hotuba ya ufunguzi wa bunge la watoto katika shule ya oysterbay mkoani manyara

Wabumbe wa Bunge la watoto Oysterbay Manyara akishangilia hoja.

Wajumbe a Bunge la watoto Oysterbay Manyara akishangilia hoja.

Waliosimama, Abdallah Waziri, Asia Mtibua na Mwalimu Gaudensia Igoshalimo wakimkaribisha Abdallah Waziri shuleni.

Mtandao wa  Marafiki wa Elimu Babati (BADENET) ulianzishwa mwaka 2012 chini ya uongozi wa Asia Mtibua, mtandao huu ulianzishwa kwa lengo la kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za elimu pamoja na kuanzisha kituo cha kupashana habari.


Moja ya mafanikio ya BADENET ni kuanzishwa kwa Bunge la Watoto katika shule ya msingi Osterbay mkoani Manyara. Bunge hili lilianzishwa kwa lengo la kuwaleta pamoja watoto waliopo shuleni na ambao wapo nje ya shule ili waweze kujadili masuala ya elimu ikiwa ni pamoja na kutafuta njia za kuweza kusikilizwa wao kama watoto. Bunge hili la watoto linajumuisha wajumbe 43 (26 wasichana na 17 wavulana) na hukutana mara 1 kwa kila mwezi. Mpaka sasa jumla ya watoto wa mitaani 19 wamerudishwa shuleni na wanasoma, wapo wanaoingia asubuhi na wengine mchana.
Leo hii Bunge la watoto Oysterbay mkoani Manyara limekutana kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili  watoto wa mitaani “Chokoraa” ili kuzungumza namna ambavyo watawawezesha  watoto hao kupata fursa ya elimu kama watoto wengine waliopo shuleni. Katika kikao cha leo bunge limefanikiwa kumrudisha shuleni mtoto Abdala Waziri ambapo alichangiwa na wabunge, marafiki wa elimu na walimu jumla ya shilingi 57,800 ili zimuwezeshe kununua mahitaji muhimu ya shule.
Mkakati wa bunge la watoto katika shule ya msingi Osterbay ni kuhakikisha kuwa kila mbunge anamrudisha shuleni mtoto yoyote ambaye yuko mtaani na kuhakikisha wanafurahia fursa ya kupata elimu ambayo ni haki yao ya msingi.
Timu ya Tafakari Time, kipindi kinachorushwa kila siku ya alhamisi kupitia ITV ilishiriki kikao cha leo kwa lengo la kujifunza uendeshwaji wa shughuli za bunge hili la watoto.

MAGUFULI AZIDI KUCHANJA MBUGA,AWATAKA WANANCHI WAWEKE IMANI KUBWA KWAKE NA KUMPA KURA NYINGI ZA USHINDI

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Njombe mjini katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa saba saba.Magufuli amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano ataendeleza juhudi zake za kujenga barabara kwa kiwango cha lami,amesema dhamira yake aliokuwa nayo ya Uwaziri wa Ujenzi katika kujenga barabara za lami katika maeneo yote hapa nchini.

Amesema tangu kupewa kuwa waziri wa ujenzi ameweza kujenga barabara  zaidi kilomita 7000 nchi nzima,ambapo ilipelekea kuongeza kuongeza pato la mfuko wa barabara kutoka bilioni 73,3 hadi kufikia bilini 866 kwa mwaka huu hivyo ameahidi akiwa rais atajenga zaidi barabara za lami.

Dkt MAGUFULI ambae anaendelea na mikutano ya kampeni za Urais mikoa ya nyanda za juu kusini , amelalamikia udanganyifu wa baadhi ya mitandao ya kijamii  na baadhi ya vyombo vya habari kuripoti  kuwa amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali ya mkoa wa mbeya wakati sio kweli.

Aidha pia Magufuli  amewaomba wananchi waweke imani kubwa kwake kwa  kumpa kura nyingi  zitakazomwezesha kuwa raisi wa awamu ya tano,na kIsha alipe fadhira hizo kwa kutatua kero zinazowakabili hasa wananchi wenye kipato cha chini.PICHA NA MICHUZI JR-NJOMBE
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Joh Pombe Magufuli akipeana mkono na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,Ndugu Phillip Mangula mara baada ya kumkaribisha mgombea huyo jukwaani kuwahutubia wananchi wa njombe na kuzinadi sera za chama chake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,Ndugu Phillip Mangula akiwashukuru wananchi wa Njombe waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa sabasaba mjini humo,ambapo pia Ndugu Mangula alimkaribisha mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kuwahutubia wananchi wa njombe na kuzinadi sera za chama chake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano
 Wananchi wa Njombe wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa sabasaba mjini Njombe.
 Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM na Mgombea Ubunge wa jimbo la Kyela,Mh Harrison Mwakyembe akiwahutubia wananchi wa Njombe jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
 Waanchi wakishangilia jambo kwenyemkutano wa kampeni wa CCM.

 Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Wanging'ombe Mh. Gerson Lwenge kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe
 Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM mgombea Ubunge wa jimbo la Wanging'ombe Mh. Gerson Lwenge kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe kwa ajili ya kuwaambia wananchi ni namna gani wataiongoza Tanzania katika awamu ya tano. 
  Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Makete Dkt Norman Msigala kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe
 MKutano wa Kampeni ukiendelea. 
 Wananchi wakisikiliza sera za mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,hayupo pichani alipowahutubia jioni ya leo mjini Njombe. 
 Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni
 Wananchi wakiwa na mabango yao ya kumsifu na kumkaribisha mgombea Urais wa CCM Ndugu John Pombe Magufuli,mara baada ya kufunga barabara alipokuwa akipita katika kijiji cha Mgagala akielekea mkoani Njombe kwenye mkutano wa kampeni
 Wananchi na Mabango yako
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Makoga katika wilaya ya Wanging'ombe mapema leo mchana.
 Wananchi  wa kijiji cha Ikonda wakimsikiliza Dkt Magufuli 
 Bango .