MD Digital

Wednesday, April 29, 2015

ACACIA YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI WAKE 510 WA MGODI WA BULYANHULU

Wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga, wakimshangilia Meneja Mkee wa mgodi huo, baada ya kumpatia zawadi ya Meneja bora wa mwaka ambaye wao wenyewe wafanyakazi walimteua. Katika hatua  nyinghine, kampuni ya Acacia imewazawadia saruji na mabati wafanyakazi wake 510 wanaofanyakazi kwenye mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu 500 kwa kuhudumu kwa muda mrefu na 10 kwa kufanya kazi kwa kuzingatia sera mpya ya kampuni hiyo ya tabia sita (Six Desired Behaviors). Utoaji wa zawadi hizo ulifanyika wakati wa sherehe za siku ya wafanyakazi duniani kwa wafanyakazi wa mgodi huo, Jumanne usiku Aprili 28, 2015. Sherehe za Mei Mosi zitafanyika kitaifa mkoani Mwanza
Michell akipongezwa na baadhi ya wafanyakazi
*****
 KAMPUNI ya uchimbaji madini, Acacia, imewazawadia wafanyakazi wake wa muda mrefu 500 na wengine 10 kwa kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juuu kwenye mgodi wake wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga.
Akikabidhi zawadi hizo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Michell Ash, alisema, katika kusherehekea sikukuu ya Wafanyakazi Duniani, maarufu kama “May Day”, Kampuni hiyo imeamua kuwazawadia wafanyakazi wake wa mgodi wa Bulyanhulu ili kutambua mchango wao.


Sikukuu ya Wafanyakazi huadhimishwa kila tarehe moja ya mwezi wa tano na mwaka huu sherehe hizo zitafanyika kitaifa mkoani Shinyanga.


Zawadi walizopatiwa wafanyakazi hao  ni mabati na mifuko ya saruji, ambapo wafanyakazi waliohudumu kwenye mgodi huo kwa mika 25, waijipatia mifuko ya saruji 100 na mabati 45 yenye thamani ya shilingi milioni 2.5, wakati wale walitumikia kampuni hiyo kwa muda wa miaka 20 walijipatia mifuko ya saruji 80 na mabati 45 yenye thamani ya shilingi milioni 2.


Wengine ni wale waliokaa kwenye kampuni hiyo kwa miaka 15, wao walipata mifuko ya saruji 60 na mabati 35 yenye thamani ya shilingi milioni 1.5, wakati waliotumikia kampuni kwa miaka 10, walijipatia mifuko 40 na mabati 25 yenye thamani ya shilingi milioni 1.
Wafanyakazi waliotumikia kampuni hiyo kwa miaka 5, wao walijipatia mifuko 20 ya saruji na mabati 15 yenye thamani ya shilingi milioni 5.

Aidha, wafanyakazi 10 kutoka idara 10 za mgodi huo ambao walizawadiwa  kutokana na kufanya kazi kwa kuzingatia tabia sita zilizowekwa na kampuni ya Acacia kwa wafanyakazi wake, kama kipimo cha utendaji bora wa kazi ambapo ni pamoja na kushirikiana na kufanya kazi kwa uwazi, kutambua ubora wa mfanyakazi na kumuwajibisha anapokengeuka, kupanga kazi na kutenda, kufanya kile ulichopanga kufanya, kufanya kazi kwa wepesi, na kujiendeleza ili kuwa bora katika utendaji wa kazi wa kila siku.
Michell akimtunuku cheti mmoja wa wafanyakazi waliohudumu kwa muda mrefu kwenye mgodi huo, mama Joyce Mgaya
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa kwenye maandamano ya kusherehekea sikukuu hiyo hapo mgodini
Michell akiwa katikan picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi waliofanyakazi kwenye mgodi huo kwa muda mrefu
Mtaalamu wa ukuzaji biashara wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, Justine McDonald, (kushoto), akimtunuku cheti cha utambuzi, mmoja wa wafanyakazi 10 bora mwaka huu, Joseph Ngowi
Afisa Mkuu wa Fedha (CFO), wa kampuni ya Acacia, Andrew Wray, akitoa hotuba yake
Mshauri mkuu wa masuala ya kiafya wa kampuni ya Acacia, Dkt. Zumbi Elvis Musiba, (kulia), akiteta jambo na mkuu wa kitengo cha biashara (Commercial), cha mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, Benedict Busunzu.
Mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu, ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, MR. LAZA, (katikati) na kundi lake pia walikuwepo
Sio kuchimba madini tu: hivi ndivyo wanavyothibitisha wafanyakazi hawa wa mgodi huo, ambao walitumbuiza kwenye sherehe hiyo
Wafanyakazi hao wakionyesha kipaji chao cha sanaa
Baadhi ya wafanyakazi wakifuatilia sherehe hiyo kwa utulivu kabisa
Michell akimpongeza mama Mgaya (kulia)
Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia anayeshughulikia udhabiti wa kampuni, Janet Reuben-Lukashingo, akiwasalimia wafanyakazi
Wafanyakazi wakifurahia jambo
Wafanyakazi wakifuatilia kwa utulivu hafla hiyo
Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Gary Chapman, (katikati), akizunumza jambo na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Michell Ash, huku Afisa Mkuu wa Fedha (CFO), wa kampuni ya Acacia inayomiliki migodi hiyo Andrew Wray,(kulia),  akisikiliza
Steven Kisyake (kulia), akifurahia jambo na mtumioshi mwenzake
Elias Kasikila, Meneja wa OE wa mgodi wa Bulyanhulu, akiongoza sherehe hioyo
Andrew Wray, (kulia), akimpongeza mfanyakazi bora wa jumla kwa mwaka huu, wa mgodi wa Bulyanhulu, Force Ngondya, kutoka kitengo cha biashara cha mgodi huo huku Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Filbert Rweyemamu akishuhudia.
Michell akimtunuku cheti Margaret Mandia kwa kuhudumu kwa muda mrefu kazini
Judith Manyalla, (kushoto), akipokea cheti cha utumishi wa muda mrefu kwenye mgodi wa Bulyanhulu.
Michell akitoa hotuba yake
Meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Acacia, Filbert Rweyemamu, akisalimia hadhira
Margareth Mageta (kushoto), akipokea cheti cha utumishi wa muda mrefu

Tuesday, April 28, 2015

NHIF YAZINDUA AWAMU YA PILI YA KAMPENI YA UHAMASISHAJI MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF).

1 Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akipokea mashuka 150 kutoka kwa Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya ya jamii CHF yaliyotolewa na mfuko huo kwa wilaya ya Kilwa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya NHIF uliofanyika katika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi, Katikati ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa mkoani Lindi Bi Fortunata Raymond.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KILWA) 2Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akiangalia mashuka 150 kutoka kwa Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF yaliyotolewa na mfuko huo kwa wilaya ya Kilwa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wananchi kujiunga afya ya jamii CHF uliofanyika katika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi, Katikati ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa mkoani Lindi Bi Fortunata Raymond.
3Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akizungumza na wananchi katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kihamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya jamii CHF. 4Rehamni Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF akizungumza na wananchi katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kihamasisha wananchi kujiunga na afya ya Jamii CHF. 6Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF na madaktari wakiandaa eneo la kuhudumia wananchi kwa upimaji wa afya wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo. 7Baadhi ya wanahabari Othman Michuzi wa Michzi Media na Fatuma kutoka Clouds Lindi wakipata taswira mbalimbali katika uzinduzi huo. 8Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akizungumza na baadhi ya wazee katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kihamasisha wananchi kujiunga na Afya ya jamii CHF baada ya kuwalipia gharama za kujiunga na mfuko huo, kulia ni Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF. 10Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akizungumza na baadhi ya wazee katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kihamasisha wananchi kujiunga na Afya ya jamii CHF baada ya kuwalipia gharama za kujiunga na mfuko huo, kulia ni Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF na katikati ni Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Bi Fortunata Raymond. 11Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi wilaya ni Kilwa. 12Baadhi ya akina mama wakishindana kukuna nazi ambapo baada ya kumaliza zoezi hilo waliunganiswa katika huduma za CHF. 13Baadhi ya madaktari wakisubiri kuanza kutoa huduma katika uzinduzi huo. 14Wananchi wakipima uzito. 15Madaktari wakiwachunguza na kuwapima afya wananchi wa kijiji cha Njia Nne kata ya Tingi wakati wa uzinduzi huo. 16Wasanii Shoti na Faida wakiburudisha wananchi huku wananchi hao wakiendelea kupata huduma katika uzinduzi huo. 17Wananchi wakiendelea kupima afya.
 18Wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa NHIF wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi huo kutoka kushoto ni Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Salvatory Okum Afisa Mfuko wa Afya ya Jamii, Fortunata Raymond Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi na Paul marenga Afisa Matekelezo na Uendeshaji NHIF mkoa wa Lindi.
************
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Bw Abdala Ulega amewakata watendaji na watoa huduma wilayani humo kuhakikisha huduma muhimu za matibabu hasa dawa zinapatina muda wote ili kuboresha huduma wilayani hapo.

Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa taifa wa bima ya afya katika halmashauri kumi nchi nzima iliyozinduliwa kata ya Tingi njia nne wilayani kilwa.

Ulega alisema serikali kupitia mifuko ya uchangiaji ya bima ya afya (NHIF) na mfuko wa afya ya jamii (CHF) imetoa fursa kwa wamiliki wa vituo vya matibabu na watoa huduma kutumia fedha za uchangiaji huduma kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vitendanishi kwa ajili ya kuboresha huduma kwa wananchi na kwamba fedha hizo sio za kulipana posho katika vikao.

Awali, mkurugenzi wa masoko na utafiti wa bima ya afya Rehani Athumani alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa kampeni hiyo inayozinduliwa itafanyika katika halmashauri nyingine kumi na hivyo kufanya jumla ya halmashauri zilizohamasisha nchi nzima kufikia halmashauri 74 katika mwaka wa fedha wa 2014/15.

Amezitaja halmashauri hizo kuwa ni Kilwa, Ruangwa, Ulanga, Korogwe na Rufiji. Nyingine tano ambazo huduma za mfuko wa CHF zitaanzishwa na kuhamasishwa katika kampeni hii ni Halmashauri ya Kaliua, Kakonko, Ushetu na Itirima.

Naye mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali la mtandao wa mifuko ya afya ya jamiii nchini (TNCHF) bibi Kidani Mhenga amewaahidi wananchi wa mikoa ya Lindi ya Mtwara kuendelea kushirikiana nao katika kutatua changamoto mbalimbali ili kuboresha huduma za matibabu kupitia mfuko wa afya wa jamii katika mikoa hiyo. Ameomba ushirikiano wa wananchi kwa ujumla kwani mafanikio ya utekelezaji wa huduma za mfuko huo zinategemea ushiriki wa wananchi katika kuchangia na kusimamia huduma. Hadi tarehe 31 machi, 2015 mfuko wa afya ya jamii ulikuwa umeandikisha jumla ya kaya 930,879 sawa na wanufaika 5,85,274.

Sunday, April 19, 2015

BALOZI LIBERATA MULAMULA AHUDHURIA MKUTANO MKUU WA WASABATO WAISHIO NCHINI MAREKANI


Mchungaji Wilbert Nfubhusa akihubiri kwenye mkutano mkubwa wa neno la Mungu wa Wasababto waishio nchini Marekani uliofanyika siku ya Jumamosi April 18, 2015 Silver Spring, Maryland. Kulia ni Michael Mwasumbi akitafsiri mahubiri kwa lugha ya Kiingereza.Mkutano huu umehudhuriwa na Watanzania kutoka majimbo mbalimbali wakiwemo wengine kutoka Tanzania.
 Mhe. Liberata Mulamula. Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiushukuru uongozi wa Wasabato nchini Marekani kwa kuweza kufanikisha mkutano wao na kuweza kumleta mchungaji Wilbert Nfubhusa na kuelezea amefurahishwa kwa makaribisho mazuri na kuwatakia mkutano mwema huku akiomba Mwenye Mungu aushushie baraka zake.

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha mdogo wake  Joycelyne Rutageruka ambaye amekuja kumtembelea Mhe. Balozi toka nyumbani Tanzania nae akitoa neno kwenye mkutano mkuu wa Wasabato wa Watanzania waishio nchini Marekani uliofanyika siku ya Jumamosi April 18, 2015 Silver Spring, Maryland.  

Nchungaji Herry Mhando akifanya mamombi maalum kabla ya kumkaribisha mchungaji Wilbert Nfubhusa kutoa mahubiri,

Mshereheshaji Magoma akifafanua jambo

Mhahubiri yakiendelea
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi