MD Digital

Thursday, December 11, 2014

MDAU ANGELA AKILIMALI NA WENZAKE WALA NONDO YA MAWASILIANO YA UMMA

Kaimu Mgukurugeni wa Uhuru FM, Angela Akilimali (katikati) akiwa na wahitimu wenzake wa Shahada ya Mawasiliano ya uma ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) katika mahafali yaliyofanyika hivi katibuni mkoani Kibaha mkoani Pwani.  Kushoto ni Hemed Mbaraka na Mganwa Nzota.
 Wanahabari wa morogoro nao walikula nondo zao katika mahafali hayo.
 Angela Akilimali akiwa na mumewe Hassan Hemedi Chamshama baada ya kumkabidhi shada la maua wakati akimpongeza.
 Toka kushoto ni Idda Mushi wa ITV/Redio One - Morogoro, Angela Akilimali wa Uhuru FM na Hana Mayige  wa TBC wakipozi kwa picha wenye furaha baada ya kula nondo zao.
 Angela akiwa na dada yake kipenzi Rose-mary Duhia aliyefika Kibaha kutoka Arusha kumpongeza mdogo wake.
 Angela akipata pongezi kutoka kwa binti yake Salma Chamshama wakati wa tafrija maalum ya kumpongeza iliyoandaliwa na familia yake.
 Picha ya familia ya Angela wakiwa pamoja na mama yao mzazi.
 Mashostito wakiwa na zawadi mkoni kabla ya kumkabidhi mhitimu.
 Wahitimu wakifurahia tafrija ...
 Wahitimu wakiwa pamoja ukumbini kusapoti Ze Big Boss.
 Mduara ulipigwa na wakazunguluka.
 Angela akizungumza kwa niaba ya wahitimu wenzake
 Wadau kutoka Uhuru FM wakifuatilia matukio ya sherehe hiyo.
 Keki ilikatwa na wahitimu walijinoma ...

 Mziki uliendelea....
 wafanyakazi wa Uhuru FM wakipiga picha ya pamoja na wahitimu.
 Neno lililotoka kwaajili ya wahitimu....
 Hongera kwa wahitimu ilitolewa...
Watu weeeeeeeee ni raha iliyoje!!

Monday, November 10, 2014

AIRTEL KUPITIA HUDUMA YA AIRTEL MONEY YAJA NA MIKOPO YA MUDA MFUPI KWA NJIA YA SIMU

 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (wa nne kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia), Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi (wa tatu kushoto), Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel, Arindam Chakrabarty (kulia) wakipiga makofi baada ya kuzindua rasmi huduma mpya ya Airtel Money Timiza, katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia) baada ya kuzindua rasmi huduma mpya ya Airtel Money Timiza mjini Dodoma jana. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi, Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel, Arindam Chakrabarty (kulia).
  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
  Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia  uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
Meneja Uendeshaji kutoka kampuni ya Airtel Tanzania,Bwa.Asupya Naligingwa akitoa maelekeo mafupi namna ya kutumia huduma hiyo mpya ya Timiza wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza, katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
Pichani kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano.
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano.
 Pichani shoto ni Mmoja wa Waimbaji mahiri wa bendi ya muziki wa dansi ya Africans Star a.k.a Twanga Pepeta,Msafiri Diof  akiwa sambamba na skwadi zima la madansa wa bendi hiyo wakitumbuiza mbele ya sehemu ya umati wa watu wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza,uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Skwea, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa Waimbaji mahiri wa bendi ya muziki wa dansi ya Africans Star a.k.a Twanga Pepeta,Msafiri Diof  akitumbuiza mbele ya sehemu ya umati wa watu wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza,uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Skwea, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
 Bendi ya Twanga Pepeta wakiwa na wadau wengine wa Airtel katika Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi
   Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia  uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana
.Kikundi cha Ngoma za asili kutoka mjini Dodoma kikitumbuiza  wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
baada ya huduma ya Airtel Money Tmiza kuzinduliwa,zikifuata shangwe kutoka kwa wageni waalikwa kama hivi pichani.
Pichani shoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi akijimwaya mwaya jukwaani wakati wa uzinduzi rasmi huduma mpya ya Airtel Money Timiza, katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.pichani kati ni Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge.
  Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia  uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
Baadhi ya Wasanii kutoka nyumba ya vipaji THT,wakitumbuiza mbele ya sehemu ya umati wa watu (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza,uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Squea, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

=======  ====== =======


·         Airtel Money Timiza, huduma mpya inayotoa mkopo wa muda mfupi kwa wateja wake kwa njia ya simu za mkononi
                       
·          Mikopo ya masharti rahisi inayotoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo  kuweza kukuza kibiashara zao.
 Dodoma Novemba 9 2014: Airtel Tanzania leo imezindua huduma itakayowawezesha wateja wa Airtel Money kupata mkopo kwa njia ya simu zao za mkononi kupitia Airtel Money. 

Huduma hiyo imezinduliwa leo rasmi na Airtel Tanzania kwa ushirikiano na AFB ambayo ni kampuni ya Kiafrika iliyobobea katika huduma ya kutoa mikopon rahisi. Huduma hii nchini Tanzania itajulikana kama "Airtel Money Timiza" ambapo lengo lake ni kuungana na serikali katika kuwezesha wanannchi na wateja wa Airtel wote kujipatia mikopo ya haraka na ya muda mfupi kwa marejesho nafuu  ya siku 7 hadi 28.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda alisema:"Uwezekano wa wananchi kuweza kupata mkopo wa muda mfupi ni motisha kubwa kwa wafanyabiashara wadogo na wakati hapa nchini .Kwa Airtel kushughulikia hitaji hili muhimu la wananchi , ni jambo la muhimu kwani wametuunga mkono serikali katika kutimiza mkakati yetu ya kuinua kipato cha wajasiriamali na kuwahamasisha kuweza kujiendeleza kibiashara. Ni dhahiri kwa upande mwingine, itasaidia kuchochea maendeleo ya kiuchumi hapa nchini"

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso ​​alisema: “Leo uzinduzi wa huduma yetu ya Airtel Money Timiza unadhihirisha dhamira  ya dhati ya  Airtel ya kutoa huduma iliyo bora na nafuu ili kugusa maisha  ya kila siku ya wateja wetu hapa Tanzania . Tunaamini huduma hii itaongeza kasi ya ukuzaji wa uchumi miongoni mwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na vikundi vya wanawake, wajasiriamali na watu binafsi. 

Pia tunaamini kwamba mikopo hii ya Airtel Money Timiza  itakuwa kichochea cha upatikanaji wa huduma za mikopo kwa  idadi kubwa ya wakazi waishio mbali na huduma za banki na hivyo kuwasaidia sana kuweza  kumudu mahitaji yao ya muda mfupi na muda mrefu."

Kwa upande wake Muanzilishi wa afb Bw, Andrew Watkins-Ball alisema “hii ni huduma ya mikopo ya kipekee tofauti na benki ambayo mara nyingi mteja hulazimika kuwa na historia ya uwekaji na utoaji katika banki hiyo, lakini mikopo ya afb inatolewa kutokana na jinsi ambavyo mteja anatumia simu.  

Kwa hiyo sasa wateja wa Airtel watapata fulsa hii ya kupata mikopo ya papo kwa hapo kwa kuwa tu wateja wakudumu na waaminifu kwa Airtel. Hii itawasaidia sana watanzania kwa mara ya kwanza kupata msaada wa haraka wa kifedha kwa haraka na nafuu, Ni imani yangu itasaidia kubadilisha mfumo wa maisha kwa watanzania wengi wenye uhitaji’

Akitoa ufafanuzi kuhusu huduma ya Airtel Money Timiza, Meneja bidhaa wa Airtel Money Bw, Moses Alphonce alisema “Airtel Money Timiza ni huduma ya kipekee, kutokana na urahisi, ni huduma iliyozingatia mahitaji ya kina kabisa ya mkopaji kwa kuondoa baadhi masharti ambayo mara nyingi yamekuwa yakikwamisha wateja kupata msaada wa haraka wa mkopo ili kujikimu”.

Ili mteja aweze kupata mkopo hakikisha tu namba yako imesajiliwa na huduma ya Airtel Money na anapaswa uwe umetumia huduma ya Airtel Money kwa kipindi cha siku 30, kisha piga *150*60 # na kuchagua TIMIZA ili ujichagulie kiasi unachotaka kukopa kulingana na mahitaji yako au kulipa mkopo.

Mkopo wa Airtel Money Timiza utatakiwa kulipwa ndani ya siku 28 kutoka kwenye  akaunti yako ya Airtel Money kama mteja mkopaji ulivyojulishwa siku alipokopa mkopo wake.

Huduma ya Airtel Money ni salama na rahisi ambayo inawawezesha  wateja kutuma na kutoa fedha kati ya simu moja ya mkononi na kwenda nyingine katika mitandao yote , kununua muda wa maongezi kwa ajili yako au ndugu jamaa na marafiki. Na pia inampa uhuru mteja kuweza kulipa bili na vile vile kununua bidhaa popote alipo.

Monday, November 3, 2014

IGP MSTAAFU PHILEMONI MGAYA ASHEREHEKEA MIAKA 85 YA KUZALIWA KWAKE

 Mara Baada ya Ibada katika Kanisa la Azania Front wakati wa  kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya
Baadhi ya waumini mbalimbali wakiwa nje baada ya Ibada
 Mkuu  wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Mstaafu Philemoni Mgaya akiwa katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake
 Keki
Waziri  Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya akimpongeza aliyekuwa IGP Philemoni Mgaya
 Mzee Timothy Msangi akieleza Historia fupi ya IGP Mstaafu Philemoni Msangi
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Alex Malasusa akitoa salam za Pongezi kwa IGP mstaafu
 Mshauri wa kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited James Rugemalira akitoa pongezi zake kwa IGP Mstaafu na kuelezea  Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Benedicta Rugemalira akitoa salam za Pongezi kwa IGP mstaafu

Mshereheshaji Joe Mgaya ambaye ni Mtoto wa IGP Mstaafu Philemoni Mgaya akisherehesha


 Waziri wa Habari na Utangazaji Fenera Mukangara  akimpa mkono wa Pongezi IGP mstaafu


 Wakiwa katika Furaha
IGP Mstaafu akipokea zawadi

IGP Mstaafu Philemoni Mgaya akikata keki huku amezungukwa na wajukuu wake



















 Watu mbalimbali wakiwa katika Sherehe hiyo




 Burudani ya nguvu

WAZIRI Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya amewaomba watanzania  kuwa na tabia ya utii wa sheria, uaminifu na uadilifu katika nafasi zao wanazozitumukia katika Taifa la Tanzania.
Msuya aliyasema hayo katika sherehe ye kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya iliyofanyika katika Hotel ya Protea , Court Yard jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu alieleza kuwa tabia aliyoionyesha Mgaya wakati wa utumishi wake serikalini inapaswa kuigwa na watanzania wote.
“Huyu ndiye Mtanzania halisi aliyelelewa vizuri kuitumikia nchi yake. Hana makuu, ni mkweli na mwadilifu. Akiahidi kufanya jambo fulani analitekeleza bila kuchelewa. Tunahitaji uwajibikaji wa namna hii,” Msuya alisisitiza.
Alisema kuwa Mgaya alikuwa kiongozi hodari ambaye alisimamia vyema kiapo na kazi zake na kipindi chake cha uongozi  alikuwa akitoa amri zinatekelezwa mara moja.
Naye Mshauri wa kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited James Rugemalira alitoa wito kwa watanzania kuendele kuunga mkono  jitihada za kuendeleza maeneo mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo viwanda.
Aliwasihi wadau kutoa ushirikiano kwa  kampuni yake inayosambaza bia aina ya Windhoek Larger na Windhoek Draught ambayo inadhamira ya kujenga kiwanda cha kuzalisha bia hizo hapa nchini.
                                       
“Tunatafuta maeneo Kilimanjaro, Tanga na Bukoba ili tuweze kujenga kiwanda hapa nchini. Tumedhamilia kufanya hivyo na tutafanya,” Rugemalira alisisitiza.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Benedicta Rugemalira aliwashukuru wananchi kwa kukubali kujumuika pamoja katika hafla hiyo na kumwomba Mzee Mgaya aendelee kuwapa mwongozo wa namna ya kuenenda katika maisha.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Alex Malasusa aliwaomba watanzania kuwa na moyo wa unyenyekevu na kujitolea kulitumikia taifa katika utumishi wao kama ilivyokuwa kwa IGP mstaaafu Mzee Mgaya.
Wageni wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Waziri wa Habari na Utangazaji Fenera Mukangara, Katibu Mkuu Msaaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Bakari Mwapachu, Balozi Antoni Nyaki na wazee wengine maarufu kama Timothy Msangi.