MD Digital

Sunday, September 7, 2014

KILIMO NI BIASHARA Ukiiona fursa usipuuzie ifanyie kazi.

Binafsi naamini kuwa kilimo ni moja ya sekta ambayo kama tutaamua kwa dhati na tukawaelekeza watu wetu kuwekeza kidogo walichonacho kwenye kilimo huku tukitumia vema ushauri wa wataalamu wa kilimo na Serikali ikatuunga mkono kwa kutuwekea sera nzuri, miundombinu imara na kutusaidia kupata soko la mazao yetu tunaweza kupiga hatua kubwa sana ya kimaendeleo kama jamii na taifa kwa ujumla.

Jukumu la kuleta maendeleo ni jukumu la kwanza la kila mwananchi anayejitambua na kutambua nafasi na wajibu wake.

Lazima tuuvae uthubutu wa kufanya yale ambayo wengine wengi wamekuwa hawayafikirii ama wanaamini hayawezekaniki.

Tanzania ni nchi inayoundwa na jamii ya walio wengi ambao ni wakulima na walio wachache ambao ni wafanyakazi. Zamani sera ya nchi ilikuwa Ujamaa na Kujitegemea chini ya Kauli mbiu "Kilimo ndio Uti wa Mgongo". Leo haijulikani kama taifa tunaamini katika sera gani rasmi. Hii ni changamoto ifanyiwe kazi.