MD Digital

Saturday, February 21, 2015

BONGO FLAVA WAMKUMBUKA MEZ B KWENYE BONANZA LA PSPF

Msanii wa muziki wa kizazi kipya "Bongo Flava, Shilole na wacheza show wake, wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka msanii mwenzao wa Bongo Flava, Mez B, mzaliwa wa Dodoma, wakati wa bonanza lililoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Februari 20, 2015. Bonanza hilo lilipambwa na michezo mbalimbali kama vile, soka, netibole, voliboli na muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiongozwa na balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto wa Mjomba band. Wasanii wengine ni pamoja na Chege na Temba na Mr. Blue. Mez B, ni mzaliwa wa mkoa wa Dodoma, ambaye alifariki leo saa tano kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma, alikokuwa akipatiwa matibabu. Anatarajiwa kuzikwa Jumatatu ijayo Februari 23.
Chege(kulia) na Temba
Wanachuo na watu wengine wakipagawishwa na muziki uliokuwa ukiungurumishwa kwenye bonanza hilo
Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Betty Mkwasa, (wapili kulia) akiwa na  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, wakwanza kulia, wakati akitoa nasaha kwa timu mbili za soka kutoka vyuo vikuu mkoani Dodoma
Maafisa wa juu wa PSPF, wakipasha misuli. Hata hivyo hawakuingian uwanjani kusakata kabumbu kutokana na muda kuwa mchache
DJ Tass, akitoa saluti kuashiria kumkumbuka Mez B
Mchezaji wa timu ya Nertiboli ya chuo cha fedha CBE mkoani Dodoma, akiruka juu kumzuia mchezaji mwenzake kutoka UDOM
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (kulia), akikabidhi jezi kwa mwakilishi wa moja ya timu za vyuo viklivyoshiriki bonanza hilo


Shilole na kundi lake
 
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Betty Mkwasa, (kulia), akiteta jambo na Meneja Masoko na mawasiliano wa PSPF, Constatina Martin
Nahodha wa timu ya soka ya Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM-DIPLOMA, Abdallah Shaaban, (kushoto, akipokea kombe la ubingwa wa soka, kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Betty Mkwasa, baada ya kuibuka washindi kwa upande wa soka kwenye tamasha hilo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu
Nasaha kwa wachezaji wa Netiboli
Mrisho Mpoto, a.k.a Mjomba, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akiburudisha wanachuo na watu wengine waluohudhuria bonanza hilo

Katika bonanza hilo, Meneja wa mpango wa uchangiaji wa hiari, Mwanjaa Seme, (kushoto), aliitumia vizuri fursa ya mkusanyiko mkubwa wa watu kusaka wanachama ambapo dereva huyu wa bodaboda alikuwa miongoni mwa waliojiunga na mpango huo.

No comments: