Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Husna Mwilima aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Arusha, Daudi Ntibenda,akifungua mkutano wa kujadili masuala ya ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi mkuu, ulioandaliwa na mtandao wa utetezi wa haki za binadamu uliofanyika jijini Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Onesmo Ole Ngulumwa, Mratibu wa Mtandao wa Kutetea Haki
za binadamu akizungumza katika mkutano huo
wa kujadili masuala ya ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi mkuu,
ulioandaliwa na mtandao wa utetezi wa haki za binadamu,kulia ni Mkuu wa
Wilaya ya Arumeru Husna Mwilima aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Arusha,
Daudi Ntibenda, kushoto Mwakilishi kutoka taasisi ya kuhamasisha masuala
ya amani nchini Marekani, Steve Hege
Mwakilishi kutoka taasisi ya kuhamasisha masuala ya amani nchini Marekani, Steve Hege akizungumza katika mkutano huo
Wadau kutoka Taasisi za kiraia
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole kulia akifatilia mkutano huo
Amani Golugwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Arusha akifatilia mkutano kwa umakini wakati mgeni rasmi akizungumza katika mkutano huo
Kiongozi wa dini akiwa anafatilia mada
Kiongozi wa dini akiwa anafatilia mada
Picha ya pamoja
Wadau wakipiga picha ya pamojana mgeni rasmi
Waandishi
wa habari hapa Nchini wametakiwa kuwaelimisha jamii juu ya umuhimu wa
amani katika nchi ya Tanzania tunapoelekea uchaguzi mkuu kwa kuandika na
kutangaza amani hali itakayosaidia uchaguzi kufanyika kwa amani
Akizungumza katika mkutano wa siku mbili wa kujadili masuala ya ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi mkuu,uliofanyika jijini Arusha mwisho mwa wiki, ulioandaliwa na mtandao wa utetezi wa haki za binadamu. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoa Arusha Husna Mwilima alisema kuwa uvunjifu wa amani una madhara makubwa sana katika nchi
Alisema kuwa vyombo vya habari vinajukumu kubwa la kuelimisha umma madhara ya vita hasa tunapoelekea uchanguzi mkuuu wa Rais,wabunge na madiwani,huku akitaka Tanzania kuiga mfano wa Kenya ambapo vyombo vya habari vya nchi hiyo vilikuwa vikitangaza na kuandika amani kipindi cha uchaguzi
Mwilima amewaomba viongozi wa vyama vya siasa, dini na taasisi zisizo za kiserikali kushirikiana kueleza wafuasi wao juu ya umuhimu wa kutunza amani wakati wa uchaguzi mkuu.
Kwa upande wake Mratibu wa Mtandao wa Kutetea Haki za binadamu Onesmo Ole Ngulumwa alisema kuwa marekebisho ya baadhi ya mambo kabla ya uchaguzi mkuu ni muhimu ili kufanyika uchaguzi salama na yenye kujali demokrasia
Pia aliongeza kuwa kwa kuwepo kwa amani itasaidia sana wananchi kupiga kura katika hali ya kiusalama zaidi
No comments:
Post a Comment