MD Digital

Wednesday, April 29, 2015

ACACIA YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI WAKE 510 WA MGODI WA BULYANHULU

Wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga, wakimshangilia Meneja Mkee wa mgodi huo, baada ya kumpatia zawadi ya Meneja bora wa mwaka ambaye wao wenyewe wafanyakazi walimteua. Katika hatua  nyinghine, kampuni ya Acacia imewazawadia saruji na mabati wafanyakazi wake 510 wanaofanyakazi kwenye mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu 500 kwa kuhudumu kwa muda mrefu na 10 kwa kufanya kazi kwa kuzingatia sera mpya ya kampuni hiyo ya tabia sita (Six Desired Behaviors). Utoaji wa zawadi hizo ulifanyika wakati wa sherehe za siku ya wafanyakazi duniani kwa wafanyakazi wa mgodi huo, Jumanne usiku Aprili 28, 2015. Sherehe za Mei Mosi zitafanyika kitaifa mkoani Mwanza
Michell akipongezwa na baadhi ya wafanyakazi
*****
 KAMPUNI ya uchimbaji madini, Acacia, imewazawadia wafanyakazi wake wa muda mrefu 500 na wengine 10 kwa kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juuu kwenye mgodi wake wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga.
Akikabidhi zawadi hizo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Michell Ash, alisema, katika kusherehekea sikukuu ya Wafanyakazi Duniani, maarufu kama “May Day”, Kampuni hiyo imeamua kuwazawadia wafanyakazi wake wa mgodi wa Bulyanhulu ili kutambua mchango wao.


Sikukuu ya Wafanyakazi huadhimishwa kila tarehe moja ya mwezi wa tano na mwaka huu sherehe hizo zitafanyika kitaifa mkoani Shinyanga.


Zawadi walizopatiwa wafanyakazi hao  ni mabati na mifuko ya saruji, ambapo wafanyakazi waliohudumu kwenye mgodi huo kwa mika 25, waijipatia mifuko ya saruji 100 na mabati 45 yenye thamani ya shilingi milioni 2.5, wakati wale walitumikia kampuni hiyo kwa muda wa miaka 20 walijipatia mifuko ya saruji 80 na mabati 45 yenye thamani ya shilingi milioni 2.


Wengine ni wale waliokaa kwenye kampuni hiyo kwa miaka 15, wao walipata mifuko ya saruji 60 na mabati 35 yenye thamani ya shilingi milioni 1.5, wakati waliotumikia kampuni kwa miaka 10, walijipatia mifuko 40 na mabati 25 yenye thamani ya shilingi milioni 1.
Wafanyakazi waliotumikia kampuni hiyo kwa miaka 5, wao walijipatia mifuko 20 ya saruji na mabati 15 yenye thamani ya shilingi milioni 5.

Aidha, wafanyakazi 10 kutoka idara 10 za mgodi huo ambao walizawadiwa  kutokana na kufanya kazi kwa kuzingatia tabia sita zilizowekwa na kampuni ya Acacia kwa wafanyakazi wake, kama kipimo cha utendaji bora wa kazi ambapo ni pamoja na kushirikiana na kufanya kazi kwa uwazi, kutambua ubora wa mfanyakazi na kumuwajibisha anapokengeuka, kupanga kazi na kutenda, kufanya kile ulichopanga kufanya, kufanya kazi kwa wepesi, na kujiendeleza ili kuwa bora katika utendaji wa kazi wa kila siku.
Michell akimtunuku cheti mmoja wa wafanyakazi waliohudumu kwa muda mrefu kwenye mgodi huo, mama Joyce Mgaya
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa kwenye maandamano ya kusherehekea sikukuu hiyo hapo mgodini
Michell akiwa katikan picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi waliofanyakazi kwenye mgodi huo kwa muda mrefu
Mtaalamu wa ukuzaji biashara wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, Justine McDonald, (kushoto), akimtunuku cheti cha utambuzi, mmoja wa wafanyakazi 10 bora mwaka huu, Joseph Ngowi
Afisa Mkuu wa Fedha (CFO), wa kampuni ya Acacia, Andrew Wray, akitoa hotuba yake
Mshauri mkuu wa masuala ya kiafya wa kampuni ya Acacia, Dkt. Zumbi Elvis Musiba, (kulia), akiteta jambo na mkuu wa kitengo cha biashara (Commercial), cha mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, Benedict Busunzu.
Mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu, ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, MR. LAZA, (katikati) na kundi lake pia walikuwepo
Sio kuchimba madini tu: hivi ndivyo wanavyothibitisha wafanyakazi hawa wa mgodi huo, ambao walitumbuiza kwenye sherehe hiyo
Wafanyakazi hao wakionyesha kipaji chao cha sanaa
Baadhi ya wafanyakazi wakifuatilia sherehe hiyo kwa utulivu kabisa
Michell akimpongeza mama Mgaya (kulia)
Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia anayeshughulikia udhabiti wa kampuni, Janet Reuben-Lukashingo, akiwasalimia wafanyakazi
Wafanyakazi wakifurahia jambo
Wafanyakazi wakifuatilia kwa utulivu hafla hiyo
Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Gary Chapman, (katikati), akizunumza jambo na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Michell Ash, huku Afisa Mkuu wa Fedha (CFO), wa kampuni ya Acacia inayomiliki migodi hiyo Andrew Wray,(kulia),  akisikiliza
Steven Kisyake (kulia), akifurahia jambo na mtumioshi mwenzake
Elias Kasikila, Meneja wa OE wa mgodi wa Bulyanhulu, akiongoza sherehe hioyo
Andrew Wray, (kulia), akimpongeza mfanyakazi bora wa jumla kwa mwaka huu, wa mgodi wa Bulyanhulu, Force Ngondya, kutoka kitengo cha biashara cha mgodi huo huku Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Filbert Rweyemamu akishuhudia.
Michell akimtunuku cheti Margaret Mandia kwa kuhudumu kwa muda mrefu kazini
Judith Manyalla, (kushoto), akipokea cheti cha utumishi wa muda mrefu kwenye mgodi wa Bulyanhulu.
Michell akitoa hotuba yake
Meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Acacia, Filbert Rweyemamu, akisalimia hadhira
Margareth Mageta (kushoto), akipokea cheti cha utumishi wa muda mrefu

No comments: