Wafanyakazi
wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani
Shinyanga, wakimshangilia Meneja Mkee wa mgodi huo, baada ya kumpatia
zawadi ya Meneja bora wa mwaka ambaye wao wenyewe wafanyakazi walimteua.
Katika hatua nyinghine, kampuni ya Acacia imewazawadia saruji na
mabati wafanyakazi wake 510 wanaofanyakazi kwenye mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu 500 kwa kuhudumu kwa muda mrefu na 10 kwa kufanya kazi kwa
kuzingatia sera mpya ya kampuni hiyo ya tabia sita (Six Desired
Behaviors). Utoaji wa zawadi hizo ulifanyika wakati wa sherehe za siku
ya wafanyakazi duniani kwa wafanyakazi wa mgodi huo, Jumanne usiku
Aprili 28, 2015. Sherehe za Mei Mosi zitafanyika kitaifa mkoani Mwanza
Michell akipongezwa na baadhi ya wafanyakazi
*****
KAMPUNI ya uchimbaji
madini, Acacia, imewazawadia wafanyakazi wake wa muda mrefu 500 na wengine 10
kwa kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juuu kwenye mgodi wake wa Bulyanhulu
ulioko wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga.
Akikabidhi zawadi hizo,
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Michell Ash, alisema, katika kusherehekea
sikukuu ya Wafanyakazi Duniani, maarufu kama “May Day”, Kampuni hiyo imeamua
kuwazawadia wafanyakazi wake wa mgodi wa Bulyanhulu ili kutambua mchango wao.
Sikukuu ya Wafanyakazi
huadhimishwa kila tarehe moja ya mwezi wa tano na mwaka huu sherehe hizo
zitafanyika kitaifa mkoani Shinyanga.
Zawadi walizopatiwa
wafanyakazi hao ni mabati na mifuko ya
saruji, ambapo wafanyakazi waliohudumu kwenye mgodi huo kwa mika 25, waijipatia
mifuko ya saruji 100 na mabati 45 yenye thamani ya shilingi milioni 2.5, wakati
wale walitumikia kampuni hiyo kwa muda wa miaka 20 walijipatia mifuko ya saruji
80 na mabati 45 yenye thamani ya shilingi milioni 2.
Wengine ni wale
waliokaa kwenye kampuni hiyo kwa miaka 15, wao walipata mifuko ya saruji 60 na
mabati 35 yenye thamani ya shilingi milioni 1.5, wakati waliotumikia kampuni
kwa miaka 10, walijipatia mifuko 40 na mabati 25 yenye thamani ya shilingi
milioni 1.
Wafanyakazi waliotumikia
kampuni hiyo kwa miaka 5, wao walijipatia mifuko 20 ya saruji na mabati 15
yenye thamani ya shilingi milioni 5.
Aidha, wafanyakazi 10
kutoka idara 10 za mgodi huo ambao walizawadiwa
kutokana na kufanya kazi kwa kuzingatia tabia sita zilizowekwa na kampuni
ya Acacia kwa wafanyakazi wake, kama kipimo cha utendaji bora wa kazi ambapo ni
pamoja na kushirikiana na kufanya kazi kwa uwazi, kutambua ubora wa mfanyakazi na kumuwajibisha anapokengeuka, kupanga kazi na kutenda, kufanya kile ulichopanga kufanya, kufanya kazi kwa wepesi, na kujiendeleza ili kuwa bora katika utendaji wa kazi wa kila siku.
Michell akimtunuku cheti mmoja wa wafanyakazi waliohudumu kwa muda mrefu kwenye mgodi huo, mama Joyce Mgaya
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa kwenye maandamano ya kusherehekea sikukuu hiyo hapo mgodini
Michell akiwa katikan picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi waliofanyakazi kwenye mgodi huo kwa muda mrefu
Mtaalamu
wa ukuzaji biashara wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, Justine
McDonald, (kushoto), akimtunuku cheti cha utambuzi, mmoja wa wafanyakazi
10 bora mwaka huu, Joseph Ngowi
Afisa Mkuu wa Fedha (CFO), wa kampuni ya Acacia, Andrew Wray, akitoa hotuba yake
Mshauri mkuu wa masuala ya kiafya wa kampuni ya Acacia, Dkt. Zumbi Elvis Musiba, (kulia), akiteta jambo na mkuu wa kitengo cha biashara (Commercial), cha mgodi
wa dhahabu wa Bulyanhulu, Benedict Busunzu.
Mfanyakazi
wa mgodi wa Bulyanhulu, ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya,
MR. LAZA, (katikati) na kundi lake pia walikuwepo
Sio kuchimba madini tu: hivi ndivyo wanavyothibitisha wafanyakazi hawa wa mgodi huo, ambao walitumbuiza kwenye sherehe hiyo
Wafanyakazi hao wakionyesha kipaji chao cha sanaa
Baadhi ya wafanyakazi wakifuatilia sherehe hiyo kwa utulivu kabisa
Michell akimpongeza mama Mgaya (kulia)
Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia anayeshughulikia udhabiti wa kampuni, Janet Reuben-Lukashingo, akiwasalimia wafanyakazi
Wafanyakazi wakifurahia jambo
Wafanyakazi wakifuatilia kwa utulivu hafla hiyo
Meneja
Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Gary Chapman, (katikati), akizunumza jambo
na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Michell Ash, huku Afisa Mkuu wa
Fedha (CFO), wa kampuni ya Acacia inayomiliki migodi hiyo Andrew
Wray,(kulia), akisikiliza
Steven Kisyake (kulia), akifurahia jambo na mtumioshi mwenzake
Elias Kasikila, Meneja wa OE wa mgodi wa Bulyanhulu, akiongoza sherehe hioyo
Andrew
Wray, (kulia), akimpongeza mfanyakazi bora wa jumla kwa mwaka huu, wa
mgodi wa Bulyanhulu, Force Ngondya, kutoka kitengo cha biashara cha
mgodi huo huku Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Filbert Rweyemamu
akishuhudia.
Michell akimtunuku cheti Margaret Mandia kwa kuhudumu kwa muda mrefu kazini
Judith Manyalla, (kushoto), akipokea cheti cha utumishi wa muda mrefu kwenye mgodi wa Bulyanhulu.
Michell akitoa hotuba yake
Meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Acacia, Filbert Rweyemamu, akisalimia hadhira
Margareth Mageta (kushoto), akipokea cheti cha utumishi wa muda mrefu























Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akipokea mashuka 150 kutoka kwa Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya ya jamii CHF yaliyotolewa na mfuko huo kwa wilaya ya Kilwa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya NHIF uliofanyika katika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi, Katikati ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa mkoani Lindi Bi Fortunata Raymond.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KILWA)
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akiangalia mashuka 150 kutoka kwa Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF yaliyotolewa na mfuko huo kwa wilaya ya Kilwa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wananchi kujiunga afya ya jamii CHF uliofanyika katika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi, Katikati ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa mkoani Lindi Bi Fortunata Raymond.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akizungumza na wananchi katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kihamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya jamii CHF.
Rehamni Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF akizungumza na wananchi katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kihamasisha wananchi kujiunga na afya ya Jamii CHF.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF na madaktari wakiandaa eneo la kuhudumia wananchi kwa upimaji wa afya wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo.
Baadhi ya wanahabari Othman Michuzi wa Michzi Media na Fatuma kutoka Clouds Lindi wakipata taswira mbalimbali katika uzinduzi huo.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akizungumza na baadhi ya wazee katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kihamasisha wananchi kujiunga na Afya ya jamii CHF baada ya kuwalipia gharama za kujiunga na mfuko huo, kulia ni Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Mh. Abdallah Ulega akizungumza na baadhi ya wazee katika kijiji cha Njia Nne wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kihamasisha wananchi kujiunga na Afya ya jamii CHF baada ya kuwalipia gharama za kujiunga na mfuko huo, kulia ni Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF na katikati ni Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Bi Fortunata Raymond.
Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kijiji cha Njia Nne Kata ya Tingi wilaya ni Kilwa.
Baadhi ya akina mama wakishindana kukuna nazi ambapo baada ya kumaliza zoezi hilo waliunganiswa katika huduma za CHF.
Baadhi ya madaktari wakisubiri kuanza kutoa huduma katika uzinduzi huo.
Wananchi wakipima uzito.
Madaktari wakiwachunguza na kuwapima afya wananchi wa kijiji cha Njia Nne kata ya Tingi wakati wa uzinduzi huo.
Wasanii Shoti na Faida wakiburudisha wananchi huku wananchi hao wakiendelea kupata huduma katika uzinduzi huo.
Wananchi wakiendelea kupima afya.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa NHIF wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi huo kutoka kushoto ni Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Salvatory Okum Afisa Mfuko wa Afya ya Jamii, Fortunata Raymond Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi na Paul marenga Afisa Matekelezo na Uendeshaji NHIF mkoa wa Lindi.