MD Digital

Friday, October 31, 2014

UN YAOKOA MAISHA YA WATOTO 3000 ZANZIBAR

DSC_0152
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari wa Zanzibar kwenye ofisi ndogo za mashirika ya Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar kuhusiana na mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na kushoto ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu.

Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Zaidi ya watoto 3000 waliokuwa wakikabiliwa na utapiamlo nchini Zanzibar sasa wapo katika hali nzuri baada ya Umoja wa Mataifa (UN)kwa kushirikiana na wadau wengine kufanikisha programu ya kusaidia kukabili utapiamlo mkali kwa watoto hao.

kauli hiyo imetolewa katika mkutano wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari uliofanyika hivi karibuni ambapo UN ilielezea mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni.

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kwamba Umoja huo ukiadhimisha miaka 69 ya uwepo wake imefurahishwa na maendeleo yaliyopatikana katika maeneo ambayo ilikuwa imejikita kusaidia kukabili umaskini,kuhakikisha utawala bora na kusaidia jamii.

Alisema pamoja na kuendeleza na juhudi za kukabiliana na utapiamlo katika visiwa vya Pemba pia Umoja huo umefurahishwa na hatua zilizofikia katika kukabiliana na vifo vya mama na mtoto na kusema ni wajibu kuhakikisha watoto hawana matatizo ya utapiamlo kwani wao ndio msingi wa taifa la sasa na lijalo.

Alisema hata hivyo upo umuhimu wa kuendelea na washirika wengine wa maendeleo kuona kwamba tatizo la utapiamlo la visiwa vya Pemba kwa watoto linamalizwa.
DSC_0177
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akielezea kufurahishwa kwake na Serikali Tanzania kwa kupigia hatua katika kutoa ajira nyingi kwa walimu kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.

Alisema pamoja na mafanikio hayo Umoja wa Mataifa unaendelea na ujenzi wa uwezo kwa baraza la wawakilishi ili kuhakikisha kwamba baraza hilo linawezesha kuwepo kwa sheria nzuri na bora na zinazotekelezeka ambazo hazikwazi kukua kwa demokrasia na ustawi wa jamii.

Aidha alisema kwa kuzingatia kwamba mwaka huu mwishoni kuna uchaguzi wa serikali za mitaa na pia uchaguzi mkuu mwakani pamoja na kura ya maoni ya katiba, Umoja huo unaendelea kufanyakazi na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kwa kuiwezesha kitaalamu kuweza kufikisha elimu ya uraia kwa wananchi.

Aidha katika masuala ya utawala bora Umoja wa Mataifa unashirikiana na taasisi za sheria kwa ajili ya kufanya mabadiliko katika mfumo wa sheria za watoto ili kuwepo na usalama mkubwa kwa watoto hasa kutokana na utamaduni uliopo visiwani kwa sasa.

Aidha alisema kwamba yamepatikana mafanikio makubwa katika sekta ya tiba na kuzuia maambukizi ya Ukimwi na kuondokana na unyanyapaa.
DSC_0121
Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Zanzibar, Talib Ussi akiuliza swali kwenye mkutano huo.

Aliwahimiza waandishi wa habari kuwa daraja la kuelezea mafanikio na pia changamoto zinazotokana na program za Umoja wa mataifa zilizolenga kusaidia maendeleo ya wananchi wa Zanzibar.

Alisema matokeo ya program ya kusaidia maendeleo ya Tanzania (UNDAP) ndiyo yatakayotumika kutengeneza UNDAP 2 ambayo inatarajiwa kuanza katikati ya mwaka 2016.

Katika mkutano huo ambapo waandishi walipata nafasi kubwa ya kuuliza masuala yanayohusu shughuli za Umoja wa Mataifa Zanzibar, Bara na duniani kwa ujumla Alvaro alizungumzia pia umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika dunia inayobadilika.

Alisema pamoja na madhumuni ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, baada ya vita kuu ya dunia ya pili mwaka 1945 ya usalama na kujenga uchumi baada ya kuharibiwa na vita yapo palepale, mabadiliko katika utendaji kwa lengo hilo hilo la usalama na maendeleo ni dhahiri.

Alisema mathalani malengo ya millennia (MDGs) ambayo yalisanifiwa kwa lengo la kuleta maendeleo duniani katika demokrasia, utawala bora na ustawi wa jamii, bado yanatakiwa kuimarishwa kupitia mpango mpya wa maendeleo SDGs wenye lengo la kutokomeza umaskini uliotopea duniani ifikapo mwaka 2030.
DSC_0060
Afisa Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni.

Alisema ni matumaini yake kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana na UN katika kuhakikisha kwamba mafanikio katika MDGs yanaendelezwa na pia kukamilisha yale ambayo hayakufikiwa kwa lengo la kutokomeza umaskini uliotopea ifikapo mwaka 2030.

Alisema mafanikio ya UNDAP kwenye utawala bora, ustawi wa jamii na uondoaji umaskini na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania, ni matokeo ya ushirikiano kati yake ya mamlaka mbalimbali nchini Tanzania na kwamba UN itaendelea kushirikiana na mamlaka hizo kuhakikisha maendeleo ya kuwezesha amani na usalama na ukuaji wa uchumi yanapatikana.

Naye Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema lengo la kukutana na waandishi wa habari wa Zanzibar lilikuwa kuangalia mafanikio na namna ambavyo program za Umoja wa Mataifa katika visiwa vya Zanzibar zinafanyakazi.

Alisema kwamba shughuli za Umoja wa Mataifa visiwani humo zinaweza tu kujulikana kwa wananchi kwa kupitia waandishi wa habari ambao wanakuwa wanajua Umoja huo unafanya nini na wapi.
DSC_0063
Mkutano kati ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari wa Zanzibar ukiendelea.
DSC_0131
Mwandishi wa habari wa TBC, Kulthum Ally, akiuliza swali kuhusiana namna Umoja wa Mataifa unavyoweza kuwasaidia Wanawake wa Zanzibar kupata nafasi za uongozi sawa na wanaume.
DSC_0192
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (waliokaa katikati), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) pamoja na Meneja wa Baraza la Habari Zanzibar, Suleiman Omar (kushoto) katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wa Zanzibar.

Thursday, October 23, 2014

PSPF YATOA ELIMU KWA WAJUMBE WA IDARA YA UTUMISHI WA WALIMU NCHINI

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu ya Polisi Morogoro, Jumatano Oktoba 22, 2014, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa wachezaji hao na wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, wanaohudhuria semina ya siku moja iliyuoandaliwa na Mfuko huo Mkoani Morogoro, Alhamisi Oktoba 23, 2014
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Neema Muro, akiwasalimia wajumbe wa semina wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na PSPF
Mjumbe wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensehni wa PSPF, kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara, akisoma kipeperushi chenye maelezo ya kina ya huduma zitolewazo na mfuko huo, wakati wa semina
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara iliyofanyika mkoani Morogoro leo Alhamisi Oktoba 23, 2014
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara iliyofanyika mkoani Morogoro leo Alhamisi Oktoba 23, 2014
Mtaalamu wa tathmini  wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, James Tenga, akitoa mada kwenye semina hiyo akielezea jinsi tathmini ya mafao inavyofanyika
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Katikati), akiwasili kwenye ukumbi wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo, kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu kutoka mikoa yote ya Tanzania bara, iliyofanyika mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ni muendelezo wa Mfuko, kutoa elimu kwa wanachama wake kutoka makundi mbalimbali
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Kulia), akisalimiana na Hafsa Mrisho, Mkurugenzi wa Utawala na  Rasilimali watu Tume ya Utumishi wa Umma, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa baadhi ya askari polisi na wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu kutoka mikoa ya Tanzania bara wanaohudhuria semina iliyoandaliwa na Mfuko huo mkoani Morogoro jana. Katikati ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akizungumza na wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na Mfuko huo mjini Morogoro Oktoba 22, 2014. Wajumbe hao wanatarajiwa kubhudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo ili kuwaelimisha walimu faida wanazoweza kupata endapo watajiunga na Mfuko huo.
 

Wajumbe wakijaza fomu za kujiunga na mpango wa fao la hiari la Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakati wa semina ya siku moja iliyowakutanisha wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu nkutoka mikoa yote nchini na kufanyika mkoani Morogoro Alhamisi Oktoba 23, 2014
Wajumbe wakijaza fomu za kujiunga na mpango wa hiari Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakati wa semina ya siku moja iliyowakutanisha wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu kutoka mikoa yote nchini na kufanyika mkoani Morogoro Alhamisi Oktoba 23, 2014
Msanii Mrisho Mpoto, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akiimba na wasanii wenzake, kwenye hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu nchini, wanaohudhuria semina ya siku moja kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo mkoani Morogoro, Oktoba 23, 2014
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Constatina Martin, akiimba sambamba na Msanii Mrisho Mpoto almaarufu kama Mjomba, wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na Mfuko huo Jumatano Oktoba 22, 2014, kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF mkoani Morogoro
Meneja wa mpango wa uchangiaji wa hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Seme, akiswasalimia wajumbe wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo, kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu semina iliyofanyika mkoani Morogoro Oktoba 23, 2014

Tuesday, October 21, 2014

KAMPUNI YA MABIBO BEER WINES AND SPIRITS LIMITED YASISITIZA UTII WA SHERIA BILA SHURUTI

 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, James Rugemalira  (kushoto), akigongeana glasi na wakili maarufu wa kampuni hiyo, Michael Ngalo.  
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Benadicta Rugemalira (Kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake. Kushoto ni Mke wa wakili, Camilo Schutte kutoka Uholanzi, Lize Schutte, Padri wa Kanisa Katoriki Parokia ya Himo, Fabian Nderumaki, Wakili Schutte na wakili kutoka Marekani, Chris Provenzano.
Katibu Mtendaji wa Kata ya Marangu Magharibi,  Rose Lyimo (anayeangalia kamera), akifurahia kinyaji bora cha windhoek na wageni wengine waalikwa.
Wadau mbalimbali wakibadilishana mawazo huku wakipata kinywaji bora cha Windhoek Draught.
Viongozi wa Kampuni ya Mabibo na mawakili kutoka Ulaya na Marekani wakipata maelezo juu ya soko la bia aina ya Windhoek kutoka kwa Meneja Mkuu wa Nymbani Hotels and Resort Mansuetha Michael (hayupo pichani). 
Wadau mbalimbali wakibadilishana mawazo mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa uongozi wa kampuni ya Mabibo namna ya kuzingatia sheria bila shuruti
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo,  Benedicta Rugemalira akimwelekeza Meneja Mkuu wa Nyumbani Hotels and Resort Mansuetha Michael namna ya kuitambua bia za Windhoek halali zinazotakiwa kuweko kwenye soko la Tanzania zenye code namba ubavuni MB66 .


Mrembo wa Hoteli ya AMEG Lodge Kilimanjaro,  Miriam Ismail akipeleka vinywaji vya windhoek kwa wateja. 
Mzee Rugemalira akitoa maelezo mafupi juu ya ubora wa bia ya Windhoek. 
Mrembo wa Hoteli ya AMEG Lodge Kilimanjaro, Miriam Isumail (kushoto), akiwa na mrembo mwenzie, Modesta Dennis.
*******
KAMPUNI ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited yenye haki pekee ya kuagiza na kusambaza kinywaji aina ya Windhoek katika soko la Tanzania imetoa wito kwa wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake kuzingatia dhana ya utii wa sheria bila shuruti. 

Wito huo ulitolewa na Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa kampuni hiyo, James Rugemalira, jana usiku katika hoteli ya Kilimanjaro Mountain Resort iliyoko katika maeneo ya Marangu, Moshi mkoani  Kilimanjaro, alipokutana na wadau mbalimbali. 

“Naomba kuwakumbusha kuwa kuna amri ya Mahakama ambayo inazuia mtu yeyote kuingiza na kusambaza Windhoek katika soko hapa nchini bila kuomba na kupata kibali kutoka Mabibo. Amri hii ni halali na inapswa ifuatwe,”  alisisitiza Rugemalira. 

Akiwa ameambatana na mawakili wake kutoka nje ya nchi na hapa nchini, Rugemalira alisisitiza kuwa bia aina ya Windhoek inayopaswa kuuzwa katika soko la Tanzania lazima iwe na alama ya MB66 na kwamba inasabazwa na kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited. 

“Hivi sasa tunatumia muda huu kutoa elimu na namna ya kuzingatia sheria bila shuruti. Lakini muda utafika na tutawashughulikia wale wote watakao kiuka amri hii,” alisema. 

Katika hafla hiyo, wageni mbalimbali walihudhuria, akiwemo Katibu Mtendaji wa Kata ya Marangu Magharibi, Rose Lyimo. 

Rugemalira aliwaomba wananchi kushirikiana na kampuni yake kwa kununua bia halali iliyolipiwa kodi ili kuweza kupanua soko ambalo litawezesha kampuni yake kuanza kuzalisha aina hiyo ya bia hapa nchini. 

Kwa sasa kampuni ya Mabibo inaagiza bia aina ya Windhoek kutoka Namibia. “Tunategemea kujenga kiwanda hapa nchini cha kuzalisha Windhoek. 

Maeneo ambayo tumeona yanafaa ni pamoja na hapa Moshi. Lakini pia tunaweza kufanya hivyo aidha Tanga au Kagera. Hivyo tushirikiane ili tujenge nchi yetu kwa pamoja na tuepuke kununua bidhaa za magendo,” alisisitiza. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

Monday, October 20, 2014

SIMBANET YAFANYA SIKU YA FAMILIA

 Kampuni ya SimbaNET (T) Linited ya jijini Dar es Salaam Jumamosi hii iliandaa bonanza la michezo lililowakutanisha pamoja wafanyakazi wa kampuni hiyo na familia zao. Siku hiyo ilikuwa ni ya kula kunywa na kuchezo michezo ya aina mbalimbali ikiwepo soka, kuvutana kamba, kuogelea, muziki na michezo mbalimbali ya watoto. Kampuni ya Seree ndio walikuwa waandaaji wa tafrija hiyo iliyofanyika kwa mafanikio makubwa katika ufukwe wa Hoteli ya Bahai Beach.
 wafanyakazi na familia zao wakichukua kifuangua kinywa mara baada ya kuwasili bahari Beach Hotel
 
 Hii ni trela tu...
Wafanyakazi wakipata kifungua kinywa.
 Watoto wakifurahia na kushiriki michezo mbalimbali ya kuogelea.
Mgeni rasmi katika siku hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa SimbaNET (T) Limited, Rakesh Kukreja akisalimia wachezaji wa timu zote akifuatana na kamisaa wa michezo hiyo Patrick Nyembela.
 Mchezo wa kuvuta kamba ulifanyika kwa makundi mbalimbali kutokana na fulana walizovaa. na Team ya weupe ndio waliibuka washindi.
 Mchezo wa soka ukiendelea ambapo Afrika Rising 'Fulana za Brown' ndio waliibuka washindi.
 Wafanyakazi kutoka Nairobi wananchi Group nao walialikwa na hapa wakifuatilia michezo hiyo na kubadilishana mawazo.
 Watoto wa wafanyakazi wa SimbaNET wakiogelea.
 Mashindano ya kuogelea nayo yalifanyika na timu ya Afrika Rising ilibuka washindi tena.
 Msosi wa mchana nao uliliwa na ulikuwa wanguvu.
 wafanyakazi wakibadiliashana mawazo.
 Wafanyakazi wakila chakula cha mchana...
 Burudani kutoka Seree Company ilitolewa na kijana chipukizi katika tasnia ya muziki.
 Hapo sasa magoma yakichezwa
 Furaha ya medali kwa African Rising...
 Wow! Keki la Birthday ilikatwa na maana Jovin na Daniela waliadhimisha siku yao ya kuzaliwa hiyo Oktoba 18.
 Burudani ya viongozi wa SimbaNET na wale wa Wananchi Group kutoka Kenya.
 Mkurugenzi wa Seree Company, Sabrina Maro (kulia) akikabidhi tuzo ya shukrani kwa kampyni ya SimbaNET kuipa heshima ya kuwaandalia bonanza hilo lililowakutanisha wafanyakazi na familia zao.
 Wafanyakazi waliopata watoto ndani ya mwaka mmoja tangu kufanyika kwa siku ya familia kama hiyo 2013 walipewa zawadi za aina mbalimbali kwa watoto wao.
Mwisho wafanyakazi na familia zao walipata nyama choma.