MD Digital

Tuesday, September 15, 2015

BIMO MEDIA YAANDAA NYERERE CUP ARUSHA

SAM_5908Mkurugenzi wa kampuni ya BIMO Media , Bertha Ismail akisoma risala katika ufunguzi wa maadhimisho ya ufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015 yaliyokuwa yakitimua vumbi katika uwanja wa Stedium jijini Arushaambapo pia yataambatana na mashindano ya kila mwaka  ya kielimu  ya uandishi wa insha,makala pamoja na uchoraji  picha juu ya masuala ya utalii  kwa wanafunzi wa shule za msingi 25 zilizopo Arusha yaliyoandaliwa na kampuni ya BIMO Media
SAM_5926Taswira katika ufunguzi wa Nyerere Cup katika uwanja wa stedium jijini Arusha
SAM_5928Mgeni rasmi Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari Josephat m.Ntabindi akiongea na vyombo vya habari pamoja na wanamichezo chini ya umri wa miaka 13,alisema kuwa mashindano hayo ni kwa ajili ya kumuenzi hayati baba wa taifa Mwl Julias Nyerere ambaye pia alikuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha michezo.
SAM_5902Meza kuu
SAM_5939Mwandishi wa TV1 Jane Edward akichukua matukio katika ufunguzi huo
SAM_5886Mgeni rasmi ambaye Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari Josephat M.Ntabindi akisalimiana na wachezaji kabla ya mechi ya TIMU ya Maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha na  timu ya AFC Arusha katikaufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015.
SAM_5893
SAM_5946Watoto wenye chini ya umri wa miaka 13 wakifanyiwa mahojiano ,aliyeshika maiki ni mmiliki wa jamiiblog Bi.Pamela Mollel
*************
TIMU ya Maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha inayoshiriki ligi daraja lakwanza imeshindwa kuonyesha makali mbele ya wadogo zao  timu ya AFC Arusha inayoshiriki ligi daraja la pili baada ya kutoka suluhu ya bao 1-1 katika ufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015.

Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Sheikh AmrI Abeid ,uliiwashuhudia maafande hao wa Oljoro wakianza kucheka na nyavu za AFC baada ya kujipatitia bao lake kupitia kwa mchezaji Swalehe Idd alilofunga kwa njia ya Penalti mnamo dakika ya 58, iliyosababishwa na mabeki wa timu pinzani kunawa mpira katika eneo la hatari.

Vijana wa AFC walionyesha juhudi zao kwa kulishambulia lango la Oljoro ambapo walifanikiwa kusawazisha bao mnamo dakika ya 88 kupitia kwa mshambuliaji wao Wandima Malechela baada ya kuachia  shuti kali lililokwenda moja kwa moja vyavuni.

Mashindano hayo yameandaliwa na kampuni ya BIMO Media yakiwa na kauli mbiu ‘Uchaguzi wa Amani  2015,ndio taifa moja kwa maendeleo ya utalii nchini’ yatazishirikisha pia timu za watoto chini ya miaka 13 ambao watachuana vikali ili kuweza kumpata mshindi ambaye atatangazwa siku ya kilele tarehe 19 mwezi huu.

Akifungua mashindano hayo Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari Josephat m.Ntabindi alieleza kuwa mashindano hayo ni kwa ajili ya kumuenzi hayati baba wa taifa Mwl Julias Nyerere ambaye pia alikuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha michezo.

“Michezo hii inawakutanisha vijana hawa  wakiwa na uwezo wao tofati  ambapo pia yatawajengea urafiki  na uhusiano mzuri baina yao  vile vile   yatawasidia kuweza kuimarisha vipaji vyao  vitakavyotumika katika kuandaa taifa lililo na vijana wenye uwezo mzuri na pia yatahamasisha utalii kwani mkoa huu una vivutio vingi.”alieleza Ntabindi.

Naye mkurugenzi wa kampuni ya BIMO Media , Bertha Ismail alisema  maadhimisho hayo yataambatana na mashindano ya kila mwaka  ya ki- elimu  ya uandishi wa insha,makala pamoja na uchoraji  picha juu ya masuala ya utalii  kwa wanafunzi wa shule za msingi 25 zilizopo Arusha.

“ Lengo ni  kuhamasisha uchaguzi wa mwaka huu kufanyika kwa amani vile vile kuhamasiha watu  kuhudhuria hifadhi za utalii zilizoasisiwa na Mwl Nyerere na tunategemea Zaidi ya wanafunzi 700 watashiriki  katika shindano hilo la isha.”ismail alifafanua.

Timu za nyota academy,Future Stars,Kijenge Youth,Rolling Stone,Young Life na palloti zitachuana na washindi watakabidiwa zawadi mbalimbali ikiwemo vikombe na fedha.

No comments: