MD Digital

Wednesday, September 30, 2015

SAMIA SULUHU AFANYA KAMPENI SIRARI

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Musoma, leo asubuhi,  kuendelea na ziara ya kufanya mikutano ya kampeni katika maeneo mbalimbali mkoani Mara. Mama Samia leo anatarajiwa kuhutubia mikutano ya kampeni Sirari,  Mwisenge,  na Sirori Simba.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Damia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenykiti wa CCM mkoa wa Mara Christopher Sanya baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Musoma, asubuhi hii.


 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimia na Mgombea Ubunge jimbo la Musoma Vijijini, Sospeter Muhongo, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Musoma leo
 Mamam Samia akisalimia baadhi ya viongozi wa CCm, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege mjini Musoma le
 
 Mama Samia akiwa na Ofisa Mwandamizi kutoka Makao makuu ya CCM Juliana Chitinka baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Musoma


Mdau akijaribu kupata picha za Mama Samia
 Msafara wa Mama Samia ukiwa njiani kwenda Sirari, Tarime mkoa wa Mara leo
Msanii wa Bongo Movie, maarufu kwa jina la Bi Mwenda, akihamasisha wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo, Sirari mkoani Mara.
 Wananchi wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Sirari, mkoani Mara
 Wananchi wakiwa na bango kuomba Mamlaka ya Mji Mdogo wa Sirari, Tarime mkoani Mara
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akimwelekeza jambo, Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini, Michael Kimbaki, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo Sirari mkoani Mara. Kulia ni Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Vijijini, Chrisopher Kangoye.
 Wananchi wakimshangilia Mama Samia kwenye mkutano wa Sirari mkaoni Mara
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwanadi wagombea Ubunge, wa majimbo ya Tarime, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo Sirari mkoani Mara. Kulia ni Chrisopher Kangoye (Tarime Vijijini) na kushoto ni Michael Kimbaki (Tarime Mjini).
 Wananchi wakipiga 'Push Up' kumuunga mkono Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassa, uliofanyika Sirari mkoani Mara.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi y CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwaaga baadhi ya viongozi, baada ya mkutano wa kampeni aliofanya leo, Sirari mkoani Mara. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

ROCK CITY MARATHON 2015 YAZINDULIWA, KUTIMUA VUMBI NOVEMBA 15

 Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye hali ya furaha mara baada ya kuzindua msimu wa saba wa mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Meneja Mkuu wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) ambao ndio warataibu wa mbio hizo Bw Erasto Kilawe (mwenye shati jeupe), Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro (wa pili kulia) na Bi Ummy Hassan kutoka idara ya Uhusiano NSSF ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa mbio hizo.
 Meneja Mkuu wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) warataibu wa mbio hizo Bw Erasto Kilawe (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa msimu wa saba wa mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.  Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa pili kushoto), Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro (wa tatu kushoto).
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa msimu wa saba wa mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa kwanza kushoto) na Bi Ummy Hassan kutoka idara ya Uhusiano NSSF ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa mbio hizo.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na waandaaji pamoja na wadhamini wa mbio za Rock City Marathon mara baada ya kuzindua rasmi msimu wa saba wa mbio hizo jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine ni (kutoka kushoto) Katibu Mkuu wa BMT, Lihaya Henry,  Meneja Mkuu wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) ambao ndio waratibu wa mbio hizo, Erasto Kilawe, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro , Bi Ummy Hassan kutoka idara ya Uhusiano NSSF ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa mbio hizo pamona na Katibu Mkuu msaidizi chama cha riadha Tanzania (RT) Bi. Ombeni  Savala .
*****************
Na Mwandishi Wetu.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi, amezindua msimu wa saba wa mbio za Rock City Marathon zitakazofanyika Novemba 15 mwaka huu kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mbio za Rock City Marathon, zinazoandaliwa na Kampuni ya Capital Plus International (CPI), kwa ushirikiano na Chama cha Riadha Tanzania (RT), pamoja na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA) zinalenga kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini na pia kukuza utalii wa ndani kupitia sekta ya michezo.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Bw. Malinzi alisema baraza linafuraha kuona makampuni binafsi yakijiingiza katika kuinua mchezo wa riadha nchini.
“Mchezo wa riadha una changamoto kubwa na tunatambua jitihada zinazoendelea kufanywa na kampuni ya Capital Plus katika kurudisha hadhi ya mchezo  huu nchini kama ilivyokuwa miaka ya sabini na themanini,” alisema.
 Alisema kuwa Tanzania itarudi kileleni katika medani za michezo duniani kama wachezaji wataandaliwa katika viwango vinavyokubalika kimataifa.
“Inashangaza kuona taifa la watu milioni 45 linawakilishwa na wanariadha wachache sana, tena katika mbio ndefu huku tukikosa wanariadha wanaoliwakilisha vyema taifa katika mbio fupi,” alisema.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mkuu kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bw. Erasto Kilawe alisema kuwa mbio hizo zimekuwa zikionyesha mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009.
 “Jiji la Mwanza limebarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali vya utalii. Jambo hili limetusukuma kuendelea kumulika vivutio vya kipekee vinavyopatikana katika ukanda wa ziwa Victoria kupitia mbio hizi,” alisema Bw. Kilawe huku akiongeza kuwa mikakati kabambe imewekwa ili kuhakikisha mbio za mwaka huu zinakuwa za mafanikio makubwa kuliko misimu iliyopita.
Alisema baadhi ya makampuni yameanza kujitokeza kudhamini mbio hizo ikiwa ni pamoja na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Precision Air, New Africa Hotel na Bank M huku makampuni zaidi yakionyesha nia ya kudhamini mbio hizo.
“Tunawaalika wadhamini waendelee kujitokeza kwa wingi ili kuzifanya mbio za mwaka huu kuwa bora zaidi,” alisema.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo ikiwa ni pamoja na wanariadha, viongozi wa vyama vya riadha, viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na wadau mbali mbali wa riadha nchini.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF , Salim Kimaro alisema kuwa shirika hilo limekuwa mstari wa mbele kudhamini mbio hizo kutokana ari yao katika kukuza hali ya michezo hapa nchini.
“Kwetu suala la michezo ni moja ya vipaumbele vyetu kutokana na ukweli kuwa michezo ni afya na pia ni sehemu ya ajira kwa vijana kwa sasa…tunaahidi kuwa mstari wa mbele katika kufaanikisha mbio hizi,’’ alisema.

Tuesday, September 29, 2015

MSAFARA WA LOWASSA WASIMAMISHWA ZAIDI YA MARA NNE WAKATI AKIWA SAFARINI KUTOKEA JIJINI TANGA KUELEKA DAR

Sehemu ya wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, wakiwa wamefunga barabara, wakimtaka Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, azungumze nao leo Septemba 29, 2015, wakati akiwa safarini kwa kuelekea jijini Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, waliofunga barabara ili azungumze nao leo Septemba 29, 2015, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.PICHA NA OTHMAN MICHUZI.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muheza wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Umati wa wakazi wa mji wa Muheza.
Ilikuwa ni furaha kwa kila aliemuona Mh. Lowassa alipokuwa akizungumza nao.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, mara baada ya kuzungumza nao, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake leo Septemba 29, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Korogwe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga leo Septemba 29, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Korogwe, Mkoani Tanga, wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga leo Septemba 29, 2015.