JUNI 16 ya kila mwaka bara
la Afrika huadhimisha siku ya mtoto wa
Afrika ikiwa ni tukio la kuwaenzi na kuwakumbuka watoto wa Soweto nchini
Afrika Kusini waliofariki wakati wa maandamano ya kutaka haki na usawa katika
elimu kutoka utawala wa Makaburi mwaka 1976.
Ni Umoja wa Nchi huru za
Afrika (OAU) hivi sasa Umoja wa Afrika (AU) mwaka 1991 ndio waliamua kuifanya
siku hiyo kuwa ya kuwakumbuka na kuwaenzi wa watoto wa Afrika kwa maadhimisho
ya kitaifa na kimataifa ambayo yanafanyika kwa kuzungumzia haki za mtoto.
Huu ni mwaka wa 24 tangu
AU iidhinishe siklu hiyo ya mtoto wa Afrika kuadhimishwa, lakini pia ni mwaka
wa 39 tangu watoto wa Soweto wapoteze maisha yao wakati wakidai haki yao.
Mwaka jana maadhimisho
hayo yalikuwa na kaulimbiu ya “Haki ya Ushiriki: Waache watoto waonekane na
wasikike” na mwaka huu pia kuna kauli mbiu yake ambayo inaogoza maadhimisho
hayo hii leo.
Pia maadhimisho ya mwaka
huu yanafanyika wakati Wakuu wa Nchi za Afrika chini ya Umoja wao AU wanakutana
nchini Afrika kusini ambapo miaka 39 iliyopita palitokea vuru na watoto
kuuwawa.
Siku ya Mtoto wa Afrika
mwaka huu inafanyika sambamba na
maadhimisho ya Miaka 25 ya Kupitishwa kwa Mkataba wa Haki za Mtoto wa Afrika na
kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Kuongeza Kasi na Jitihada Zetu za Pamoja Kutokomeza
Ndoa za Utotoni Afrika.”
Kama mzazi ambaye nami ni
nawatoto wa kike na hata wakiume pia ninaunga mkono kauli mbiu ya mwaka huu.
Mimba za utotoni katika
nchi nyingi za Afrika bni tatizo kubwa ambalo hakika linahitaji sauti ya pamoja
ya kulikemea ili kuliondoa kama si kulimaliza kabisa.
Vita vya mara kwa mara
katika nchi nyingi za Afrika ni moja ya vitu ambavyo husabisha watoto wengi wa
kike kupata mimba za utotoni kutokana nakubakwa na hata wengine kunajisiwa.
Lakini hapa Tanzania sisi
tuna amani ya kutosha na utulivu ambao kama tutautumia ipasavyo hili tunaliweza
kuliondoa achilia mbali umasikini unaozikabili kaya zetu na kupelekea watoto
hasa washule kulubuniwa na malaghai wachache na kuishia katika mimba.
Lakini wapo wazazi
waliokosa hekima na busara ambao huwaoza binti zao wakiwa na umri mdogo na
wengine hata bila kuwashirikisha watoto hao.
Jana Chama Cha Waandishi
wa Habari Wanawake (Tamwa) kupitia Mkurugenzi Mtendaji wa wake, Valerie Msoka,
walitoa tamko na kusema kuwa ni ukiukwaji wa haki za mtoto wa kike kutokana na
kuwa ndoa nyingi zinapangwa na kujikita zaidi katika makubaliano kati ya
anayetaka kuoa na wazazi wa mtoto wa kike na kushindwa kuhakikisha mhusika mkuu
anaridhika.
Msoka alisema kuwa ndoa za
umri mdogo zimeonesha kuongezeka kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita ambapo
takwimu zinaonesha kuwa barani Afrika na Asia vitendo hivyo vinaongoza.
Utafiti wa Watu na Afya
nchini Tanzania (TDHS) wa mwaka 2010, ulibawastani wa watoto wanne katika kila
watoto 10 wa kike wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18.
Kwa mujibu wa utafiti huo,
inakadiriwa kuwa asilimia 37 ya wanawake wa umri kati ya miaka 20 na 24 kwa
mwaka 2000/2011 waliolewa au kuwa na mahusiano ya ndoa walipofikia umri wa miaka
18.
Mmomonyoko wa maadili
katika jamii ndio chanzo kikubwa pia ya kukosekana kwa maadili ambayo
yanapelekea watoto wetu hawa kuingia katuika vitendo hivyo kabla ya wakati.
Ndoa zinapokuwa na
migogoro ambapo baba na mama wanakosa kuelewana kama kuna mtoto wa kike na
kiume basi watoto wa kike huishia kuozwa katika umri mdogo kwa tama ya mzazi
mmoja.
Hivyo basi ni vyema wazai
tukadumisha amani katika ndoa zetu na kuwapa malezi mema watoto wetu ili wakue
kwa misingi iliyobora.
Umefika wakati sasa wa
jukumu la malezi ya watoto wetu kuto liacha kwa wazazi pekee bali liwe la jamii
nzima kama ambavyo sisi tulilelewa hapo zamani na tukakua kwa maadili. (Porojo hii pia imechapishwa katika gazeti la Habarileo Juni 16,2015 kama WAZO).
No comments:
Post a Comment