MD Digital

Monday, March 30, 2015

NYERERE, MANDELA KUPEWA TUZO ZA HESHIMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TUZO YA JAMII ITAKAYOTOLEWA TAREHE 13 APRIL 2015 KATIKA UKUMBI WA JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVENTION CENTRE, JIJINI DAR ES SALAAM



MGENI RASMI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete



WAGENI WAALIKWA:

Mara baada ya Hafla ya Tuzo ya Jamii ambapo Washindi wote watapewa Tuzo na Mgeni Rasmi, Kutakuwa na Dhifa ya Kitaifa ya Tuzo ya Jamii ambayo itahudhuriwa na wageni wafuatao:



  • Wapewa Tuzo,
  • Familia za wapewa Tuzo,
  • Viongozi Waandamizi wa Serikali,
  • Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania,
  • Viongozi wa vyama vya siasa na kijamii na Wafanyabiashara,
  • Taasisi zisizo za kiserikali,
  • Watu Mashuhuri na
  • Wawakilishi kutoka makundi yenye mahitaji maalum ambapo kwa mwaka huu watawakilishwa na Watu wenye Ulemavu wa Ngozi-Albino



MUHIMU:

Tanzania Awards International Ltd imepanga kufanya hafla ya utoaji wa Tuzo ya Jamii na kisha Dhifa ya Kitaifa ya Tuzo ya Jamii siku ya tarehe 13 ya mwezi April ya kila mwaka kwa malengo ya kuadhimisha Kumbumbuku ya siku ya kuzaliwa  Baba wa Taifa,  Hayati Mwalimu Julius Kambarege Nyerere.



Kuhusu Tanzania Awards International Limited

Tanzania Awards International Limited ni kampuni iliyosajiliwa kisheria nchini Tanzania kwa Malengo ya Kufanya tafiti mbalimbali, Kutoa ushauri wa kisheria na kijamii, kuandaa na kuratibu matukio pamoja na Uandaaji na Utoaji wa Tuzo Ya Jamii.



Maana ya Tuzo ya Jamii

Tuzo ya Jamii ni Tuzo inayotolewa kwa Taasisi na Watu binafsi kutokana na Mchango na Jitihada zao katika kusaidia na kutetea maslahi ya Jamii.





Malengo ya Tuzo ya Jamii

  • Kutambua, Kuthamini, Kuunga Mkono na Kutoa Tuzo kwa Taasisi au Mtu Binafsi kutokana na Mchango na Jitihada zake katika kusaidia na kutetea maslahi ya Jamii.



  • Kuikumbusha Jamii kuona umuhimu, kujali na Kuunga Mkono jitihada zinazofanywa na Taasisi au Mtu Binafsi katika kuleta Ustawi na Maendeleo ya Jamii



VIPENGELE VYA TUZO YA JAMII 2015

Vipengele vya Tuzo ya Jamii, hubadilika kila mwaka kulingana na aina na matokeo ya Utafiti unaofanywa na Tanzania Awards International Limited. Kwa mwaka huu (2015), Tuzo ya Jamii itakuwa na Vipengele Vikuu vinne (4) vifuatavyo:



  1. Tuzo ya Jamii 2015
  2. Tuzo ya jamii –Tuzo ya Heshima
  3. Tuzo ya Jamii ya Haki za Binadamu
  4. Tuzo ya Jamii kwa Mwanasiasa mwenye mafanikio katika siasa za Tanzania



UFAFANUZI WA KILA KIPENGELE CHA TUZO YA JAMII 2015



  1. Tuzo ya Jamii 2015

Tuzo hii itatolewa kwa Taasisi au Mtu Binafsi kutokana na mchango na jitihada zake katika kusaidia na kutetea Jamii.



Mshindi wa Tuzo hii ya Jamii atapatikana kwa:



(a)   Mhusika mwenyewe kuwasilisha vielelezo au ushahidi wa mchango wake huo kwa Jamii

AU

(b)   Kwa jamii kupendekeza jina la mhusika kupitia mitandao ya kijamii

AU

(c)    Kwa Kamati ya Tuzo ya Jamii kufanya utafiti, kuchambua na kuteua jina moja miongoni mwa yale yaliyopatikana kupitia kipengele (a) na (b)



Mshindi wa Tuzo ya Jamii 2015 atatangazwa rasmi siku ya Hafla ya Tuzo ya Jamii itakayofanyika tarehe 13 April 2015 katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre, Jijini Dar es Salaam



2. Tuzo ya Jamii-Tuzo ya Heshima

Watakaopewa Tuzo ya Jamii-Tuzo ya Heshima ni:

(a)  Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na



(b) Hayati Nelson Mandela –Rais wa Kwanza Mzalendo wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini

Tuzo hii ya Heshima kwa mwaka huu itatolewa kwa Waasisi hao wawili kutokana na Jitihada na Mchango wao wa kipekee na uliotukuka katika kutetea na Kulinda Maslahi ya Wanyonge







3. Tuzo ya Jamii ya Haki za Binadamu

Tuzo hii inatolewa kwa Taasisi au Mtu Binafsi kutokana na Mchango na Jitihada zake katika Kuelimisha, kulinda, kutetea na Kuimarisha Utawala Bora nchini Tanzania



Vigezo vinavyotumika kwa mwaka huu katika kumpata mshindi wa Tuzo ya Jamii ya Haki za Bianadamu, ni hivi vifuatavyo:



·         Weredi wa Taasisi au Mtu Binafsi katika kufanya uchunguzi, Utafiti na kutoa taarifa zake kwa uhuru, pasipo upendeleo wowote kwa Serikali, Chama, Kikundi au mtu Binafsi

·         Mchango wa Mtu Binafsi au Taasisi katika Kuelimisha Jamii,  kulinda, kutetea na kuhamasisha juu ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania.



·         Mchango wa Mtu Binafsi au Taasisi katika kulinda, kuhifadhi na kuhamasisha juu Amani, utulivu, Usalama wa Raia na Mali zao na Utii wa Sheria kwa ujumla



  1. Tuzo ya Jamii ya Mwanasiasa Mwenye Mafanikio katika siasa za Tanzania



Mshindi wa Tuzo hii atatangazwa siku ya hafla ya Tuzo ya Jamii baada ya mwanasiasa husika kupigiwa kura nyingi kupitia mtandao wa Push mobile ambapo mpigaji wa kura anatakiwa aende sehemu ya kuandika ujumbe mfupi wa maneno katika simu yake ya Mkononi na kuandika namba ya Mwanasiasa husika, alafu anatuma namba hiyo kwenda 15522.



Vigezo vitakavyotumiwa na wapiga kura kupitia namba 15522 ni hivi vifuatavyo:



  • Uadilifu, Uaminifu, Heshima na Utii kwa Jamii na sheria za nchi kwa Amani ya nchi yetu



  • Jitihada binafsi katika kulinda na kutetea Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar, Umoja wa Kitaifa na Kijamii



  • Uzoefu wa Uongozi wa Umma, Taasisi za Kimataifa na Mchango wake kwa Jamii.



  • Matarajio, Mipango na nia ya Dhati ya Kuleta Maendeleo na Mafanikio kwa Watanzania



Orodha ya Wanasiasa wanaowania Tuzo ya Jamii ya Mwanasiasa Kijana na Mtu Mzima Mwenye Mafanikio katika siasa za Tanzania imepatikana baada ya wanajamii kupendekeza mara nyingi jina la Mwanasiasa husika kupitia Mtandao wa Push Mobile na mitandao mingine ya kijamii. Kamati ya Tuzo ya Jamii, baada ya kupitia majina yote yaliyopendekezwa kupitia mbalimbali ikiwemo Push Mobile, imepata orodha ifuatayo:



WATU WAZIMA

JINA LA MWANASIASA
NAMBA YA KUMPIGIA KURA
MHE. MIZENGO PETER PINDA
MM01
MHE. PROF. SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO
MM02
MHE. DR. WILBROD PETER SLAA
MM03
MHE. ASHA-ROSE MTENGETI MIGIRO
MM04
MHE. SAMIA HASSAN SULUHU
MM05
MHE. JAMES FRANCIS MBATIA
MM06
MHE. DR. JOHN POMBE MAGUFULI
MM07
MHE. DR. HARRISON GEORGE MWAKYEMBE
MM08
MHE. PROF. IBRAHIM HARUNA LIPUMBA
MM09
MHE. STEPHEN MASATU WASIRA
MM10
MHE. BALOZI LIBERATA MULAMULA
MM11
MHE. BENARD KAMILIUS MEMBE
MM12
MHE. EDWARD NGOYAYI LOWASSA
MM13



VIJANA

JINA LA MWANASIASA
NAMBA YA KUMPIGIA KURA
MHE. JANUARY YUSUPH MAKAMBA
MK01
MHE. ZITTO ZUBERI KABWE
MK02
MHE. MWIGULU LAMECK NCHEMBA
MK03
MHE. HALIMA JAMES MDEE
MK04
MHE. SAADA SALUM MKUYA
MK05
MHE. LAZARO SAMUEL NYALANDU
MK06
MHE. ESTHER AMOS BULAYA
MK07
MHE. UMMY ALLY MWALIMU
MK08
MHE. NAPE MOSES NNAUYE
MK09
MHE .MBONI MHITA
MK10
MHE. DAVID ZACHARIA KAFULILA
MK11
MHE. VICKY PASCHAL KAMATA
MK12
MHE. JOHN JOHN MNYIKA

RAIS KIKWETE ZIARANI MAREKANI KWA MWALIKO WA UMOJA WA MATAIFA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili, Machi 29, 2015 amewasili jijini New York, Marekani kwa mwaliko wa Umoja wa Mataifa.
Miongoni mwa mambo mengine, Rais Kikwete amefunguia rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa, na Jumatatu Machi 30, 2015 amealikwa kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa la Uchumi na Jamii (ECOSOC - UN).
Rais Kikwete akilakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa Dkt Mahadhi Juma Maalim alipowasili jijini New York, Marekani. 
Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa WAZIRI wa Kazi na Ajira, Mhe. Gaudensia Kabaka anayefuatiwa na Waziri wa Fedha wa Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee ...
Jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akikata utepe kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akisalimiana na baadhi ya  Wawakilishi wa Kudumu kutoka nchi mbalimbali walioalikwa kushuhudia ufunguzi wa  jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akisalimiana na wakandarasi wa ujenzi  wa  jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalumu Mhe.Naomi Mwakyoma Kaihula katika ufunguzi wa  jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akifunua pazia kama ishara ya kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete na pamoja na Mwakilishi wa Kudumu Katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na wageni waakikwa wakipiga makofi mara alipofungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa Dkt Mahadhi Juma Maalim (kulia) na Mwakilishi wa Kudumu Katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi mara alipofungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akisalimiana na maafisa wa Wizara ya Mambo y Nje na Ushirikiano wa Kimataifa baada ya  kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akikagua ofisi katika jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Kushoto ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi 
Rais Kikwete akiangalia picha za waliopata kuwa Wawakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa baada ya  kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akiangalia picha za waliopata kuwa Wawakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa baada ya  kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Nyuma yake ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi 
Rais Kikwete akisaini kitabu cha wageni baada ya kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Akiangalia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi 
Rais Kikwete akisalimiana na wafanyakazi kwenye ofisi hizo mara alipofungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Joseph Msami wa Raido ya Umoja wa Matifa Idhaa ya Kiswahili kwenye ofisi hizo mara alipofungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akipiga picha na wageni mara alipofungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akipiga picha na Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika katika Umoja wa Mataifa, Balozi Amina Salum Ali   baada ya kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akihutubia mara alipofungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akihutubia mara alipofungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa nchi mbalimbali za za Afrika katika Umoja wa Mataifa baada ya kufungua  rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri, Wabunge, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Mbele kushoto) na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman (kulia)baada ya kufungua  rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani

Rais Kikwete akatika picha ya pamoja na wafanyakazi wa ubalozini hapo  baada ya kufungua  rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akatika picha ya pamoja na wafanyakazi wa ubalozini hapo  baada ya kufungua  rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akatika picha ya pamoja na wenzanwa wafanyakazi wa ubalozini hapo  baada ya kufungua  rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akatika picha ya pamoja na wafanyakazi wakandarasi wa ujenzi wa jengo baada ya  kulifungua  rasmi jengo hilo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akatika picha ya pamoja na wanajumuiya wa Tanzania wanaoishi Marekani w baada ya kufungua  rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akatika picha ya pamoja na baadhi ya Wa-Tanzania wanaoishi Marekani w baada ya kufungua  rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mwakilishi wa matawi ya CCM MArekani Bw. Isaac Kibodya na Mkewe  baada ya kufungua  rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mwakilishi wa matawi ya CCM Marekani Bw. Isaac Kibodya na Mkewe  baada ya kufungua  rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na baadhi ya Watanzania waishio Marekani