MD Digital

Tuesday, July 14, 2015

TUSILAUMIANE, POLISI JICHUNGUZENI NA UVAMIZI HUU



USIKU wa kumkia jana Jeshi la Polisi lilipata pigo kubwa kufuatia vifo vya askari wake 4 na mwingine kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kuvamia kitio Kikuu cha Polisi Stakishari Ukonga.

Kituo hiki ni kikubwa kwani ni Kituo Kikuu cha Wilaya ya Kipolisi ya Ukonga, katika Kanda maalum ya Dar es Salaam ambacho kina wajibika katika mkoa wa Kipolisi Ilala.

Naandika hapa huku nikiwa na majonzi na huzuni kubwa kufuatia vifo vya wapendwa wetu hawa. Pia walikufa raia watatu huku mmoja akihisiwa kushiriki katika tukio hilo na kuuwawa na wenzake hao.

Hili la Ukonga Stakishari limetokea wakati bado hatujasahau yaliyotokea katika vituo vingi vya Polisi kama Newala, Ikwiriri, Kimanzichana na Bukombe ambapo iliripotiwa jumla ya silaha 41 zimeporwa na baade 32 kupatikana lakini pia askari zaidi ya 5 kuuwawa. 

Tukio hili la Ukonga Stakishari limetokea ikiwa imepita miezi minne tangu Rais jakaya Kikwete alipozungumzia wimbo hilo la mashambulizi kwenye vituo vya polisi nchini.

Rais Kikwete akihutubia taifa miezi minne iliyopita, alisema kuwa  polisi wanachunguza sababu ya uvamizi huo. Bila shaka na ninaamini kuwa uchunguzi huo ulisha baini sababu ya uvamizi huo.

Lakini jana tumeshuhudia tena jinamizi hilo la uvamizi na uwaji wa Polisi vituoni nchini ukianza tena baada ya kimya cha muda mrefu na wananchi tuliamini kudhibitiwa kwa hali hiyo.

Japo kuwa Wakuu wa Chombo hicho cha Ulinzi wa raia na mali zake wanatoa hofu kwa wananchi kuwa watulivu na amani lakini, nitakuaje na amani kama chombo cha kunitunzia hiyo amani kinashambuliwa na walinzi hao wa amani kuuwawa ilhali wanamafunzo na silaha za kutosha?.
 
Kituo cha Polisi si sehemu ya masihara hata kidogo hasa ukizingatia unyeti wa Jeshi la Polisi hapa nchini.

Ipo haja ya Polisi wakiwa vituoni humo wakae kwa hadhari kubwa, na pia kuwa tayari kwa lolote wakati wowote.

Jeshi la Polisi ni mhimili wa nchi katika suala zima la ulinzi wa raia na mali zao,  hivyo tunatarajia kuona juhudi za makusudi zikifanyika kuhakikisha vituo vyote vya jeshi hilo siyo tu vinalindwa, bali pia vinawekewa mazingira ya kuwawezesha askari polisi kufanya kazi zao bila hofu ya kuvamiwa. 

Ni kweli vipo vituo ambavyo havina mazingira rafiki ya kazi na si salama lakini kwa kituo kikubwa kama Stakishari Ukonga, inatubidi kuamka sasa.

Si wakati wa kulaumiana au kunyoosheana vidole, lakini kitendo cha kuvamiwa na majambazi na kuporwa silaha, huku baadhi ya askari wake wakiuawa na wengine wakiachwa na vilema vya maisha si jambo dogo, mi nadhani kuna sehemu pia ndani ya jeshi letu tunapaswa kuliangalia, ama ni askari kujisahau na kumwamini kila mtu au hujuma miongoni mwa askari.

Nasema hujuma kwa maana ya kwamba, nirahisi mtu kufika kituo cha polisi na kufanya atakayo lakini kufika hadi chumba maalum cha kuhifadhia silaha na kuzichukua kama zake kirahisi tu nasema iko namna.

Chumba hicho daima huamini kuwa ni chumba kilicho na ulinzi mkali na pia huwa na milango imara ambayo itamfanya mtu yeyote anaetaka kufanya uhalifu humo kukamatwa kabla ya kufikia adhma yake hiyo. 

Ijapo kuwa vituo vya polisi ni nyumba ya wahalifu lakini siamini kama wahalifu hawa tuwafikishapo vituoni humo huwatembeza kila kona ya majengo yetu kiasi siku wakija wanajua kabisa hamari ni wapi na funguo hukaa wapi au mlango ule ukiupiga teke unafunguka.

Huenda wanakuwa na wenyeji, katika hili IGP Mangu, na maofisa wako hamna budi kuchunguzana kimaadili na mienendo ya askari wetu siku hadi siku na kubaini wale walio katika mstari na walio nje.

Wakati umefika sasa wa jamii kutoa taarifa za uhalifu kwa Jeshi la Polisi kwa lolote ambalo unalihisi si salama. 
POROJO Hii imechapishwa leo katika Gazeti la HABARILEO 
kama WAZO LA MWANDISHI.

Monday, July 6, 2015

Wanahabari tujitoe kwa mambo yanayotuhusu tuache kutumika



MWANDISHI wa habari ni mtu muhimu sana katika jamii, na wakati mwingine amekuwa akitambulika kama Mhimili wa nne usio rasmi wa serilali, ukiacha Bunge, Mahakama na Serikali.

Waandishi wapo mstari wa mbele sana kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za maendeleo, kupaza sauti juu ya kero mbalimbali zilizopo katika jamii hizo na hata watatuzi wa hizo kero ama serikali au makundi mengine katika jamii hizo kuona na kutafuta ufumbuzi wake.

Mwandishi wa habari ni mtu ambaye huitumia kalamu yake ama kujenga kitu au mtu na mtu huyo ama kitu hicho kuonekana ni bora zaidi kuliko vyote lakini pia kalamu hiyo hiyo Mwandishi anaweza kuitumia kuboa kabisa kile alichokijenga kwa sifa nyingi na jamii kuona huyu ndio mtu.

Hebu ona sasa hivi mwandishi wa habari hasa Yule anayeaminika katika chumba fulani cha habari alivyo ‘lulu’ katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani.

Kila mtu mwenye nia ya kutaka kugombea kuwania moja ya nafasi za uongozi anahaha kupata mwandishi ambaye kama si kuamuandika vizuri gazetini au kumtangaza vizuri na hao wapiga kura wake watarajiwa wakamsoma ili wamchague.

Ndio! Na waandishi wa wazuri wapo wengi sasa wadau hapa wanazidiana kete tu na mtu kutoka huku kwenda huku. Wapo wanaofanya kazi hiyo ya kuwapamba na kuwafagilia watu ilimradi tu aione kesho yake bila kujadi maadili au laa  lakini wapo wanaoifanya kazi hiyo kwa kuzingatia maadili.

Mwandishi wa habari amekuwa mbele sana katika kufanya mambo ya watu, lakini akijisahau yeye mwenye matatizo lukuki yanayo mkabili. Hebu angalia wafanyakazi wa kampuni fulani wagome kuhusiana na maslahi duni wanayopata au manyanyaso kwa mwajiri wao uone kesho watakavyo andika magazetini na kutangaza, lakini wamesahau kuwa wao ndio watu wa mwisho katika maslahi na hata hayo madogo wanayotakiwa kuyapata hawayapati kwa wakati.

Hivi sisi waandishi tumelogwa! Na kama ndio basi aliyetuloga hiyo tunguli kaitupa baharini na na mganga mwenye kujua tiba yake kafa. Haiwezekani tumeshindwa kujikingia kifua, ni waoga au nini kinatusibu hata kushindwa kupigania maslahi yetu? Jamani haya maslahi tunashindwa hata kusaidiana nako tunashindwa?

Juzi Kundi fulani la waandishi lisilo rasmi liliamua kuendesha kampeni ya kutafuta fedha za kuwasaidia wenzao wanaumwa maradhi mbalimbali ikiwepo saratani.

Nilifika katika tamasha hilo lililopewa jina la ‘Media Car Wash for Cancer’ pale viwanja vya Leaders  Dar es Salaam nikiwa mshereheshi (MC) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic alikuwa mgeni rasmi, pia tulikuwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.

Viongozi hao walifika kutunga mkono katika harambee hiyo, mapema akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisikitishwa sana na hali za waandishi wa habari jinsi wanavyofanya kazi katika mazingira magumu, wakiwa na maslahi duni pasipo na mikataba ya ajira. Ndio! Wengi wetu tunaishi kama vibarua na hata hao walio ajiriwa au kuwa na mikataba ni duni.

Makonda aliomba ridhaa ya Mkuu wa Mkoa kama vipi alibebe suala la kufuatilia maslahji ya wanahabari kama alivyofanikiwa kwa madereva wan chi hii, ambao leo wamepota mikataba inayoeleweka na mbioni kupatiwa bima za afya wao na familia zao.

Naamini kabisa Makonda sakata la madereva alilijua kupitia waandishi na vyombo vya habari.

Katika harambee hiyo waandishi hawakujitokeza kwa wingi wao kama tunavyojuana idadi yetu. Tumeshindwa kujitokeza kucheza ngoma yetu wenyewe je tumtarajie nani atoke acheze? Sidhani kama Makonda atatosha bila sisi wenyewe kuonesha nia ya kujisaidia.

Licha ya umasikini wetu lakini wengi wetu tuna magari ambayo yangeoshwa pale na kupata fedha, mbona pikipiki yangu Mkuu wa Mkoa na Mkuu wake wa Wilaya waliiosha na kuingiza sh 150,000/=. Wachache waliokuja nawapongeza na waendelee na moyo huo huo, tukijua fika leo kwao kesho kwetu.

Wanahabari wakati umefika sasa wa kila mmoja wetu kujitoa katika mambo yetu na kuacha kutumiwa na watu kwa faida zao. Tumekuwa watumwa wa wanasiasa hivi sasa lakini ngoja washinde kama hata simu au sms yako atajibu. 
Porojo hii imechapishwa kwa mara ya kwanza katika gazeti la Habarileo Julai 05,2015 kama Wazo la Mwandishi.

MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA AWAFUTURISHA WAFANYAKAZI


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akifuturu pamoja na wageni waalikwa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC yeye mwenyewe.
Waandazi wa futari hiyo iliyofuturiwa jijini Dar es Salaam wakiendelea na maandalizi siku ya tukio.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akifuturu pamoja na wageni waalikwa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC yeye mwenyewe.
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Chediel Msuya akionyesha umahiri namna ya kunywa maji katika dafu wakati wa futari hiyo iliyoliwa makao makuu ya NHC.
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu wa Shirika la Nyumba la Taifa, James Rhombo akishiriki futari kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa, David Misonge Shambwe, Almasi Kassongo na Elias Msese wakishiriki futari kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Samweli Metilli na Adolf Kasegenya wakishiriki futari kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo.
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo
Baadhi ya washiriki wa futari iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya NHC (NHC PLACE) jijini Dar es slaan Julai 3, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu pia walialikwa kwenye futari hiyo

Thursday, June 25, 2015

LOWASSA AZIDI KUJIPATIA WADHAMINI LUKUKI, WANACCM 42, 405 WAMDHAMINI MKOANI MANYARA LEO

Msafara wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa ukipokelewa kwa shangwe na wanaCCM na Wananchi wa Mji wa Babati, Mkoani Manyara, wakati alipowasili kwenye mji huo kusaka wadhamini  watakaomuwezesha kutapa ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Sehemu ya Wakazi wa Mji wa Babati wakimshangilia Mh. Lowassa pale walipomuona.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa na baadhi la viongozi wa CCM Mkoa wa Manyara wakati alipowasili kwenye Ofisi Kuu za Chama hicho, Mjini Babati leo Juni 25, 2015.
 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akimsalimia Kijana Jacob Jeremiah ambaye ni mlemavu wa miguu, alipokutana nae nje ya Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Manyara, iliopo Mjini Babari leo Juni 25, 2015, wakati akiwa katika ziara ya kusaka wadhamini  watakaomuwezesha kutapa ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (wa pili kulia), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha,Onesmo Ole Nangole pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu wakitembea sambamba na wanaCCM wengine kuelekea kwenye uwanja wa CCM Wilaya ya Babati, tayari kwenda kukabidhiwa fomu za Wadhamini, leo Juni 25, 2015. 
Safari ikiendelea.
Mh. Lowassa akisaini kutabu cha Wageni cha Ofisi ya CCM Wilaya ya Babati, Mkoani Manyara.
Muimbaji wa Nyimbo za Injili, Bahati Bukuku akiimba moja ya nyimbo zake wakati akiwasalimia WanaCCM na Wananchi wa Mji wa Babati, Mkoani Manyara leo Juni 25, 2015.
Sehemu ya WanaCCM na Wananchi wakazi wa Mji wa Babati Mkoani Manyara, wakiwa kwenye Uwanja wa CCM Wilaya ya Babati.
Mjumbe wa NEC kutoka Wilaya ya Mlele, Mkoani Katavi, Kampala Thomas Maganga akiwasalimia wanaCCM wa Mji wa Babati Mkoani Manyara.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akisema neno wakati akiwasalimia wanaCCM na Wananchi wa Mji wa Babati, Mkoani Manyara leo Juni 25, 2015.
WanaCCM wa Babati Mkoani Manyara.
Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Mh. Kiseryi Chambiri akizungumza jambo wakati Mh. Lowassa alipofika kuomba udhanini wa WanaCCM wa Mji wa Babati, Mkoani Manyara leo Juni 25, 2015.
Meza kuu.
Tabasamu la Mh. Lowassa baada ya maneno ya Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Mh. Kiseryi Chambiri.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Mh. Kiseryi Chambiri.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Edward Lowassa akipokea fomu ya udhamini kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Babati Mjini, Daniel Ole Porokwa, leo Juni 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 42, 405 wa Mkoa wa Manyara.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Edward Lowassa akizungumza wakati akiwashukuru wanaCCM wa Mkoa wa Manyara, waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Lowassa amepata wadhamini 42, 405 , Mjini Babati Mkoani Manyara leo, Juni 25, 2015.