MD Digital

Saturday, February 21, 2015

BONGO FLAVA WAMKUMBUKA MEZ B KWENYE BONANZA LA PSPF

Msanii wa muziki wa kizazi kipya "Bongo Flava, Shilole na wacheza show wake, wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka msanii mwenzao wa Bongo Flava, Mez B, mzaliwa wa Dodoma, wakati wa bonanza lililoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Februari 20, 2015. Bonanza hilo lilipambwa na michezo mbalimbali kama vile, soka, netibole, voliboli na muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiongozwa na balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto wa Mjomba band. Wasanii wengine ni pamoja na Chege na Temba na Mr. Blue. Mez B, ni mzaliwa wa mkoa wa Dodoma, ambaye alifariki leo saa tano kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma, alikokuwa akipatiwa matibabu. Anatarajiwa kuzikwa Jumatatu ijayo Februari 23.
Chege(kulia) na Temba
Wanachuo na watu wengine wakipagawishwa na muziki uliokuwa ukiungurumishwa kwenye bonanza hilo
Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Betty Mkwasa, (wapili kulia) akiwa na  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, wakwanza kulia, wakati akitoa nasaha kwa timu mbili za soka kutoka vyuo vikuu mkoani Dodoma
Maafisa wa juu wa PSPF, wakipasha misuli. Hata hivyo hawakuingian uwanjani kusakata kabumbu kutokana na muda kuwa mchache
DJ Tass, akitoa saluti kuashiria kumkumbuka Mez B
Mchezaji wa timu ya Nertiboli ya chuo cha fedha CBE mkoani Dodoma, akiruka juu kumzuia mchezaji mwenzake kutoka UDOM
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (kulia), akikabidhi jezi kwa mwakilishi wa moja ya timu za vyuo viklivyoshiriki bonanza hilo


Shilole na kundi lake
 
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Betty Mkwasa, (kulia), akiteta jambo na Meneja Masoko na mawasiliano wa PSPF, Constatina Martin
Nahodha wa timu ya soka ya Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM-DIPLOMA, Abdallah Shaaban, (kushoto, akipokea kombe la ubingwa wa soka, kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Betty Mkwasa, baada ya kuibuka washindi kwa upande wa soka kwenye tamasha hilo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu
Nasaha kwa wachezaji wa Netiboli
Mrisho Mpoto, a.k.a Mjomba, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akiburudisha wanachuo na watu wengine waluohudhuria bonanza hilo

Katika bonanza hilo, Meneja wa mpango wa uchangiaji wa hiari, Mwanjaa Seme, (kushoto), aliitumia vizuri fursa ya mkusanyiko mkubwa wa watu kusaka wanachama ambapo dereva huyu wa bodaboda alikuwa miongoni mwa waliojiunga na mpango huo.

Thursday, February 19, 2015

MKUTANO WA NNE WA PSPF WAMALIZIKA LEO MJINI DODOMA

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi, akitoa mada, kuhusu benki hiyo inavyoweza kuwasaidia wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kutokana na ushikiano wa kibiashara baina ya taasisi nhizo mbili, wakati wa mkutani mkuu wa nne wa wanachama na wadau wa PSPF mjini Dodoma. Mkutano huo wa siku mbili umefungwao Alhamisi Februari 19, 2015.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akisikiliza kwa makini majadiliano ya wanachama na wadau wa Mfuko huo wakati wa mkutano mkuu wa nne wa wanachama na wadau wa PSPF mjini Dodoma ,leo Alhamisi Februari 19, 2015.
Kaimu mkurugenzi wa fedha na utawala wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Yahaya Ally, akitoa taarifa ya fedha ya Mfuko huo wakati wa mkutano wa nne wa wanachama na wadau wa PSPF, mjini Dodoma. Mkutano huo ulioanza Februari 18, umefungwa leo Alhamisi Februari 19, 2015
Dkt.Bill Kiwia, akijibu hoja mbalimbali za washiriki wa mkutano mkuu wa nne wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF kuhusu ushindani wa mifuko ya hifadhi ya jamii na tahadhari ya kuchukua a,kitolea mfano wa Tanzania mjini Dodoma leo Alhamisi Februari 19, 2015
Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa nne wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakifuatilia mkutano huo leo, wakati wa ufungaji
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Neema Muro, akitoa mada kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko huo kwa wanachama wake, wakati wa mkutano mkuu wa nne wa wanachama na wadau mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya mkutano mkuu wa nne wa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakiongozwa na Meneja wa Masoko na Mawasiliano wa Mfuko huo, Costantina Martin (wapili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanikisha mkutano huo kwa mafanikio makubwa. Mkutano huo umemalizika leo Alhamisi Februari 19, 2015

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Gabriel Silayo, akitoa mada kuhusu uwekezaji katika sekta mbalimbali uliofanywa na Mfuko huo, wakati wa mkutano mkuu wa nne wa wanachama na wadau wa PSPF mjini Dodoma. Mkutano huo umemalizika leo
Kikundi cha wasanii mkoani Dodoma, kikitoa burudani kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa nne wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, mjini Dodoma. Mkutano huo umemalizika leo

Wednesday, February 4, 2015

OLOLOSOKWAN WAPIGWA MSASA KUKITUMIA VYEMA KIJIJI CHA DIJITALI

DSC_0066
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiendesha mjadala kwa wanakijiji wa Ololosokwan na vijiji vingine vinavyozunguka kijiji hicho,viongozi wa halmashauri, viongozi wa kimila, viongozi wa vijiji na wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya, elimu na uchumi ikiwa ni maandalizi ya kuupokea mradi wa kijiji cha kidigitali Ololosokwani wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
DSC_0095
Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta (kulia) akiwa kwenye majadiliano na baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu na nini kifanyike kuboresha sekta ya elimu kwa ujumla katika kijiji hicho na kuishirikisha halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro katika maandalizi ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali.
********
Na Mwandishi wetu, Ngorongoro
SHIRIKA la Elimu ,sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, limeanza maandalizi ya kuumilikisha mradi wa kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa wananchi wa kijiji hicho kwa kuendesha warsha ya siku mbili ya kutambua vipaumbele vya wananchi vitakavyoingizwa katika mradi huo.

Vipaumbele hivyo ni katika elimu, afya na uchumi. Warsha hiyo ilishikirikisha wanakijiji wa Ololosokwan na vijiji vingine vinavyozunguka kijiji hicho,viongozi wa halmashauri, viongozi wa kimila, viongozi wa vijiji na wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya, elimu na uchumi.

Katika majadiliano yao wananchi walitambua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ambazo zina uhusiano wa moja kwa moja na mazingira na mfumo wa utamaduni walionao wakazi wa eneo hilo.

Wakazi hao ambao ni wafugaji wenye kuheshimu mila na utamaduni wa kimasai na mfumo wa maisha wamesema kwamba lugha inayotumika katika kufundishia ni tatizo na ingawa wana shule mbili za msingi na sekondari lugha ya Kiswahili ni tatizo na wakifika sekondari lugha ya kiingereza nayo inakuwa tatizo.

Aidha walisema kutokana na wazazi kutokuwa na elimu hawaoni sababu ya kuwafanya watoto wao wenye maarifa makubwa kwenda shule na badala yake hao wanaoelewa vitu hupelekwa kuchunga au wale wenye umri mdogo wa kike huolewa.

Warsha hiyo pia ilibainisha tatizo la afya ya wanawake na watoto, ndoa za utotoni na magonjwa ya zinaa ya kuambukiza.

Kijiji hicho cha digitali ambacho ni nadharia ya Samsung katika kurejesha faida kwa umma kitakuwa na huduma mbalimbali ambazo zikiunganishwa na haja ya wananchi zitasaidia kubadili maisha ya wamasai na kuondokana na utegemezi wa mifugo pekee na kutambua thamani yao katika rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

Warsha hiyo ambayo imesimiwa na wataalamu kutoka UNESCO imelenga kuwafungua macho na kuwashirikisha wananchi kuhusu mradi huo mkubwa wa aina yake nchini na duniani.
Kijiji cha dijitali nchini Tanzania ni cha nne cha kwanza kikiwa nchini Afrika Kusini, kingine Gabon na Ethiopia.

Kijiji hicho ili kiwe endelevu wananchi wanaohusika wanatakiwa kuelewa mradi huo kuweka vipaumbele vyao na kuangalia jinsi ya kutumia mradi huo katika kukabili changamoto zinazowakabili kwa sasa.

Katika majadiliano kwenye ngazi za elimu wananchi walielezea haja ya kushawishi wamasai kuanza kujifunza Kiswahili na Kiingereza ili kuweza kufuatilia kwa karibu masomo na pia kuwepo kwa sheria ndogo ili kuzuia utoro wa wanafunzi kwa ajili ya kwenda kuchunga mifugo na pia kuolewa mapema kwa mabinti.

Mathias Herman, mratibu wa program za Afya , UNESCO, alisema kwamba pamoja na kwamba kijiji hicho kitakuwa na zahanati na huduma za mawasiliano ya tiba (telemedicine) hamasa kubwa inatakiwa kutolewa ili wananchi waweze kutumia huduma hizo kwani kwa sasa wamejikita zaidi huduma za waganga wa jadi.

Alisema katika warsha kulielezwa kuwa kukosekana kwa madaktari katika zahanati zilizopo kijijini hapo kumefanya watu wengi kuendelea kuamini waganga wa jadi na kujifungulia huko hali ambayo imezaa kuwapo kwa idadi kubwa ya wanawake wanaokufa wakati wa uzazi na pia watoto wasiopata chanjo.

“Wakifika hakuna madaktari hawawezi kuamini huduma hii wakati kuna waganga wa kienyeji na wakunga wa kienyeji” alisema Mathias na kuongeza kuwa katika warsha ilihimizwa kwamba watu watambue tatizo lililopo la kiafya linalosababishwa na mfumo wa mazingira na maisha ya wafugaji na kuhakikisha kwamba huduma zinazoletwa zinatumiwa vyema.

Aidha alisema kuwapo kwa kiwango kikubwa cha maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ndoa za utotoni na mimba katika umri mdogo ni sehemu ya matatizo ambayo yanaaminika kwamba yanaweza kutanzuliwa kwa kutolewa elimu na kushawishi wakubwa wa mila kutambua nafasi zao na elimu ya kisasa katika kushughulikia changamoto za kiafya.

“mila na heshima kwa wakubwa wa mila kumefanya wamasai kutegemea tiba za asili na mfumo wa asili wa kuendesha maisha bila kujua athari kwao ziwe hasi au chanya” alisema Mathias kauli iliyoungwa mkono na Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues ambaye alisema kunahitajika sana ushirikiano wa jamii, viongozi, wazazi kuhakikisha kwamba kijiji kinafanikiwa na kuwa cha kupigiwa mfano.

Kijiji cha Ololosokwan kilichopo Loliondo, wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kikiwa na watu 9000 kupitia mradi huo kitapewa pia mbinu za kuimarisha soko la utalii, kulitambua na kulitumia kwa manufaa yao na pia elimu ya ubunifu ambayo itawafanya wanawake wanaotengeneza urembo mbalimbali kuweza kumudu soko la utalii na la kawaida.


Aidha mradi huo utafikisha umeme na elimu kwa njia ya Tehama huku, elimu hiyo ya Tehama ikikusudiwa kutumika kutoa elimu ya darasani kwa wanafunzi ambao wapo machungani.
Mfumo wa wamasai ambao umejengwa katika utamaduni na kuthamini mifugo unatakiwa kubadilishwa kwa wazazi kupewa elimu ya kuwawezesha kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao.
DSC_0103
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph akiendesha mjadala na baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan kuhusiana mradi wa kijiji cha kidigitali na kuuboresha ili kutatua matatizo ya wananchi pamoja na kuwapata taarifa za maendeleo kupitia redio jamii ya Loliondo FM inayofadhiliwa na UNESCO ikiwa ni katika maandalizi ya kuupokea mradi huo wa kijiji hicho unaotarajiwa kuwasili hivi karibuni kijijini hapo.
DSC_0145
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akiongoza mjadala wa nini kifanyike katika kuboresha sekta ya afya na changamoto zinazowakabili wanakijiji wa Ololosokwan kwa ajili ya maandalizi ya kuupokea mradi wa kijiji cha Kidigitali unaoendeshwa na UNESCO kwa kushirikiana na kampuni ya Ki-elektroniki ya Samsung unaotarajiwa kuwasili mapema mwezi februari kijijini hapo. Wa pili kushoto ni Mratibu wa Taifa wa tiba asilia na mbadala katika Idara ya Tiba Wizara ya Afya na ustawi wa jamii. Dkt Liggy Vumilia.
DSC_0226
Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta akiwasilisha kazi ya kikundi chake baada ya kujadiliana na wanakijiji wa Ololosokwan katika kuboresha sekta ya elimu ikiwa ni maandali ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali kinachotarajiwa kuwasili hivi karibuni kijijini hapo.
DSC_0124
Mmoja wa washiriki wa kikundi kilichokuwa kikijadili masuala ya utamaduni na utalii akiandika changamato mbalimbali zinazowakabili wakinamama wakimasai wanaofanya biashara za urembo wa kimasai kwa watalii wanaotembelea hifadhi ya Ngorongoro.
DSC_0089
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akishiriki kwenye mjadala na wanakijiji wa kijiji cha Ololosokwan katika maandalizi ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali unaotarajiwa kuwasili mapema mwezi februari kijiji hapo.
DSC_0231
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisaini mkataba wa kukabidhiwa ardhi iliyotolewa na serikali ya kijiji kwa ajili ya mradi wa kijiji cha kidigitali huku tukio hilo likishishudiwa na uongozi wa juu wa serikali ya kijiji, wataalam kutoka UNESCO na halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro pamoja na wanakijiji.

Wednesday, January 7, 2015

LAURIAN CHOLOBI NA FELISTER SANGA WALIVYOMEREMETA SIKU YA NDOA YAO

 ILIKUWA ni siku ya furaha sana kwa Laurian Cholobi na mkewe Felister Sanga wakiwa na furaha baada ya kufunga ndoa yao takatifu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Immaculata parokia ya Upanga, Dar es Salaam hivi karibuni na baade katika tafrija iliyofanyika ukum,bi wa Urafiki. 
 Photos Production: MD Digital Company 
+255 755 373999/+255 717002303 (Mroki Mroki).
 wapambe wakimeremeta
  maharusi wakitoka kanisani...
 maharusi wakipiga picha na wasimamizi wao.
 Laurian Cholobi Panguwinga akivutana na biharusi na wapambe wake.
 Nduigu jamaa na maharusi.
 Maharusi wakiingia ukumbini
 Bwabna harusi laurian Cholobi akifurahi na DC wa Bahi, Betty Mkwasa.
 Ndugu wa bwana harusi wakiwa ukumbini..
 Waalikwa wakiwa ukumbini.
 Bi harusi akiwa na Felister akiwa mama mkwe wake
 Picha ya familia ya maharusi
  Keki ilikatwa na ndugu wote pamoja na maharusi.
Mroki Mroki 'Father Kidevu' - akipiga picha na maharusi pamoja na wasimamizi wao.