MD Digital

Sunday, November 2, 2014

MSONDO NGOMA MUZIC BAND YATIMIZA MIAKA 50

Safu ya waimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma ikiongozwa na Nguli Shaaban Dede (katikati) wakifanya vitu vya mbele ya mashabiki wao lukuki waliofika kwenye Viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar.

 Bendi Kongwe ya Muziki wa Dansi hapa nchini iliyodumu kwa miaka 50 toka kuanzishwa kwake mwaka 1964,Msondo Ngoma Music Band imesherehekea jubilei yake hiyo iliyofanyika Novemba 1,2014 katika viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha mashabiki wake lukuki kutoka sehemu mbali mbali.

Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo ya kusherehekea Jubilei ya miaka 50 ya Bendi ya Msondo Ngoma,alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye aliweza kuwatunuku vyeti vya heshima wanamuziki mbali mbali walioitumia Bendi hiyo toka ilipoanzishwa mpaka sasa.
Mpiga Tumba wa Msondo Ngoma akifanya yake.
Hassan Moshi William (mtoto wa Marehemu TX Moshi Willian) akionyesha uhodari wake kiasi kwamba hata pengo la mzee wake kuhisi limezibwa.
Rapa wa Bendi ya Msondo Ngoma,Roman Mng'ande akifanya mambo.
Baba la Mababa,Mzee Said Mabela akiendeendelea kuzikonga nyoyo za Mashabiki wa Msondo.
Abdul Ridhwan "Panga mawe"

Shaaban Dede akiimba kwa hisia.
Juma Katundu.
Mkaanga chipsi wa Msondo akizicharaza kweli kweli.
Wakongwe wengine hawa wakiimba wimbo wao wa Tanzania.
Ilifika zamu ya Twanga Pepeta na huyu si mwingine bali ni Saleh Kupaza.
Kalala Junior.
Kalala na Msafiri Diof wakienda sawa na Mashabiki wao.
Msafiri Diof.........
Taswira juu ya Taswira katika Sherehe za Miaka 50 ya Msondo Ngoma.
Kalala Junior na Saleh Kupaza wakifanya yao ikiwa ni sehemu ya Usindikizaji wa Sherehe za Miaka 50 ya Msondo Ngoma.
Madansa wa Twanga Pepeta Juu kwa Juu
Mandela wa Twanga Pepeta 
Wacheza Shoo wa Twanga Pepeta ni Hatariiiiiiiii...
Wadau wakijipatia taswira muhimu.
Msondo Umekolea kwa Mdau huyu.
Wadau.
Romariiiiiiiiiii Romariooooooo na Trampet yake.
Mdau akichukua taswira muhimu.
Dar Modern Taarab "watoto wa mjini" wakisindikiza sherehe hizo.
Msondo Ngoma iliyozikonga nyoyo za Mashabiki wao hakuna mtu kukaa chini.
Msongo Ngoma staili.
Bendi ya Vijana Jazz ilikuwepo kuwasindikiza kwakongwe wenzao.
Bint wa Kiongozi wa Bendi ya Vijana Jazz Marehemu Hemed Maneti akitoa burudani safii.
Hakuna kazi ngumu kama ya kupuliza hii kitu,inahitaji pumzi kubwa sana kama wanavyoonekana wanamuziki hawa wa Vijana Jazz.
Nyomiiii.
MC Zomboko.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea Cheti cha heshima kutoka kwa Muwakilishi wa Mfuko wa PSPF,Abdul Njaidi ambao ni sehemu ya Wadhamini wa Bendi hiyo ikiwa ni sehemu ya heshima kwa Mh. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wake mkubwa kwa wasanii mbali mbali hapa nchini.Cheti hicho kimetolewa na Bendi ya Msondo Ngoma.Picha Zote na Othman Michuzi.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima Kiongozi wa Bendi ya Msondo Ngoma,Mzee Said Mabela.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima mpiga solo hodari wa Bendi ya Msondo Ngoma,Abdul Ridhwan "Panga mawe"
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel akimkabidhi Cheti pamoja na fedha taslim sh. Laki 5,Mke wa Marehemu Mzee Muhidin Maalim Gurumo katika hafla hiyo ya kutimiza miaka 50 ya kuanziswa kwa Bendi hiyo.
Mmoja wa Waanzilishi wa Bendi hiyo,John Simon (Kapten Mstaafu) akizungumza machache pamoja na kutoa historia fupi ya kuanza kwa bendi hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti pamoja fedha taslim sh. Mil. 5,Hassan Moshi William (mtoto wa Marehemu TX Moshi Willian) kwa niaba ya baba yake.
Mtangazaji Mkongwe hapa nchini na mwenye historia na Muziki wa Tanzania,Masoud Masoud (kulia) akionyesha moja ya CD za bendi ya Msondo Ngoma zilizokuwa zikinadiwa kwenye sherehe hizo mbele ya Wadhamini.

DK KINGWANGALA ASHIRIKI BONANZA LA MBIO ZA AMANI DAR ES SALAAM LILILOSHIRIKISHA KLABU ZA MAZOEZI

 Mbunge wa Nzega mkoani Tabora ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamiti ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, Dk. Hamisi Kingwangala(watatu kulia mstari wa mbele) akishiriki katika mazoezi ya viungo na umoja wa vilabu vya mazoezi Dar es Salaam (FAITA) mara baada ya kupokea bonanza na mbipo za amani zilizofanyika jana Dar es Salaam kuanzia Uwanja wa Taifa hadi viwanja vya Mnazi Mmoja. 
 Mbunge wa Nzega mkoani Tabora ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamiti ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, Dk. Hamisi Kingwangala(kulia) akipokea vilabu m,balimbalimbali vya joging vya Dar es salaam vilivyoshiriki bonanza na mbio za amani zilizofanyika leo kuanzia Uwanja wa Taifa hadi viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam chini ya uratibu wa FAITA Joging & Sports Club.
  Mbunge wa Nzega mkoani Tabora ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamiti ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, Dk. Hamisi Kingwangala(watatu kulia mstari wa mbele) akishiriki katika mazoezi ya viungo na umoja wa vilabu vya mazoezi Dar es Salaam (FAITA) mara baada ya kupokea bonanza na mbipo za amani zilizofanyika jana Dar es Salaam kuanzia Uwanja wa Taifa hadi viwanja vya Mnazi Mmoja.
 Wana joging wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
 Viongozi na Mgeni rasmi Dk. Hamisi Kingwangala wakishiriki kuimba wimbo huo wa taifa.
 Wimbo ukiimbwa
Mazoezi ya viongo yaliendelea ....
Mgeni rasmi Mbunge wa Nzega mkoani Tabora ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamiti ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, Dk. Hamisi Kingwangala(kushoto) na Mwenyekiti wa MBT, Dionis Malinzi wakisaini vyeti.
Wanamichezo hao pia walipata fursa ya kuachangia damu katika Kitengo cha Damu salama cha serikali.
Mbunge wa Nzega mkoani Tabora ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamiti ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, Dk. Hamisi Kingwangala akitoa hotuba yakea ambapo alihimiza vilabu hivyo vya joging kuanzisha Saccos ili waweze kusaidiana kiuchumi.
Mbunge wa Nzega mkoani Tabora ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamiti ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, Dk. Hamisi Kingwangala akiwa na wana joging.
Mbunge wa Nzega mkoani Tabora ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamiti ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, Dk. Hamisi Kingwangala akimkabidi Mwenyekiti wa BMT, Dionis Malinzi chezti huku Mwenyekiti wa zamani wa BMT, Kanali Mstaafu Idd Kipingu akishuhudia (kulia).
Vyeti vikitolewa kwa Klabu za Joging zilizoshiriki bonanza hilo ikiwa ni Bonanza la tatu kufanyika tangu FAITA ianzishwe.
Mbunge wa Nzega mkoani Tabora ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamiti ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, Dk. Hamisi Kingwangala akisaidiwa na Afisa Muuguzi kutoka kitengo cha Damu Salama, Seline Sahani, kuchangia damu baada ya kupokea mbio za Klabu za joging Dar es Salaam zilizoshiriki mbio za amani.