MD Digital

Monday, October 20, 2014

SIMBANET YAFANYA SIKU YA FAMILIA

 Kampuni ya SimbaNET (T) Linited ya jijini Dar es Salaam Jumamosi hii iliandaa bonanza la michezo lililowakutanisha pamoja wafanyakazi wa kampuni hiyo na familia zao. Siku hiyo ilikuwa ni ya kula kunywa na kuchezo michezo ya aina mbalimbali ikiwepo soka, kuvutana kamba, kuogelea, muziki na michezo mbalimbali ya watoto. Kampuni ya Seree ndio walikuwa waandaaji wa tafrija hiyo iliyofanyika kwa mafanikio makubwa katika ufukwe wa Hoteli ya Bahai Beach.
 wafanyakazi na familia zao wakichukua kifuangua kinywa mara baada ya kuwasili bahari Beach Hotel
 
 Hii ni trela tu...
Wafanyakazi wakipata kifungua kinywa.
 Watoto wakifurahia na kushiriki michezo mbalimbali ya kuogelea.
Mgeni rasmi katika siku hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa SimbaNET (T) Limited, Rakesh Kukreja akisalimia wachezaji wa timu zote akifuatana na kamisaa wa michezo hiyo Patrick Nyembela.
 Mchezo wa kuvuta kamba ulifanyika kwa makundi mbalimbali kutokana na fulana walizovaa. na Team ya weupe ndio waliibuka washindi.
 Mchezo wa soka ukiendelea ambapo Afrika Rising 'Fulana za Brown' ndio waliibuka washindi.
 Wafanyakazi kutoka Nairobi wananchi Group nao walialikwa na hapa wakifuatilia michezo hiyo na kubadilishana mawazo.
 Watoto wa wafanyakazi wa SimbaNET wakiogelea.
 Mashindano ya kuogelea nayo yalifanyika na timu ya Afrika Rising ilibuka washindi tena.
 Msosi wa mchana nao uliliwa na ulikuwa wanguvu.
 wafanyakazi wakibadiliashana mawazo.
 Wafanyakazi wakila chakula cha mchana...
 Burudani kutoka Seree Company ilitolewa na kijana chipukizi katika tasnia ya muziki.
 Hapo sasa magoma yakichezwa
 Furaha ya medali kwa African Rising...
 Wow! Keki la Birthday ilikatwa na maana Jovin na Daniela waliadhimisha siku yao ya kuzaliwa hiyo Oktoba 18.
 Burudani ya viongozi wa SimbaNET na wale wa Wananchi Group kutoka Kenya.
 Mkurugenzi wa Seree Company, Sabrina Maro (kulia) akikabidhi tuzo ya shukrani kwa kampyni ya SimbaNET kuipa heshima ya kuwaandalia bonanza hilo lililowakutanisha wafanyakazi na familia zao.
 Wafanyakazi waliopata watoto ndani ya mwaka mmoja tangu kufanyika kwa siku ya familia kama hiyo 2013 walipewa zawadi za aina mbalimbali kwa watoto wao.
Mwisho wafanyakazi na familia zao walipata nyama choma.

Sunday, September 7, 2014

KILIMO NI BIASHARA Ukiiona fursa usipuuzie ifanyie kazi.

Binafsi naamini kuwa kilimo ni moja ya sekta ambayo kama tutaamua kwa dhati na tukawaelekeza watu wetu kuwekeza kidogo walichonacho kwenye kilimo huku tukitumia vema ushauri wa wataalamu wa kilimo na Serikali ikatuunga mkono kwa kutuwekea sera nzuri, miundombinu imara na kutusaidia kupata soko la mazao yetu tunaweza kupiga hatua kubwa sana ya kimaendeleo kama jamii na taifa kwa ujumla.

Jukumu la kuleta maendeleo ni jukumu la kwanza la kila mwananchi anayejitambua na kutambua nafasi na wajibu wake.

Lazima tuuvae uthubutu wa kufanya yale ambayo wengine wengi wamekuwa hawayafikirii ama wanaamini hayawezekaniki.

Tanzania ni nchi inayoundwa na jamii ya walio wengi ambao ni wakulima na walio wachache ambao ni wafanyakazi. Zamani sera ya nchi ilikuwa Ujamaa na Kujitegemea chini ya Kauli mbiu "Kilimo ndio Uti wa Mgongo". Leo haijulikani kama taifa tunaamini katika sera gani rasmi. Hii ni changamoto ifanyiwe kazi.

Monday, August 11, 2014

RIDHIWANI KIKWETE AZINDUA KISIMA CHA MAJI, LAMBO KATIKA KIJIJI CHA JAMII YA WAFUGAJI CHA MBALA,CHALINZE

 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete akionozana na akina mama wa jamii ya kimasai waliobeba maji waliyoyateka baada ya mbunge huyo kuzindua kisima cha maji katika Kijiji cha Mbala, Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani jana. Kisima hicho pamoja na lambo la kunyweshea mifugo vimejengwa na Kanisa la Wasabato kwa gharama ya sh. mil. 76. Kushoto ni Kiongozi wa mradi huo, Joseph Chagama na nyuma yake ni Askofu wa Kanisa la Wasabato Jimbo la Mashariki,Mark Malekana. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Ridhiwani Kikwete akifunua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima hicho. Kushoto ni Askofu wa Kanisa la Wasabato Jimbo la Mashariki,Mark Malekana.
 Ridhiwani akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa jamii ya kimasai baada ya kuzindua kisima hicho.
 Mama mwingine wa Jamii ya Kimasai akitwisha ndoo ya maji na Ridhiwani Kikwete

 Ridhiwani Kikwete akifungua maji ikiwa ni ishara ya kuzindua lambo la kunyweshea mifugo katika Kijiji cha Mbala kinachokaliwa kwa asilimia kubwa na jamii ya wafugaji
 Ng'ombe wakitoka kunywa maji kwenye lambo hilo
 Watoto wa kimasai waonja maji ya kwenye lambo baada ya uzinduzi
 Kwaya ya Amkeni ya Kanisa la Wasabato la Mbala, ikitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kisima cha maji uliofanywa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, katika Kijiji cha Mbala, Chalinze, mkoani Pwani jana. Kanisa hilo limejengwa na Kanisa la Wasabato kwa gharama ya sh. mil. 76. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia) akishiriki katika maombezi
Kwaya ya Kanisa la Wasabato la Manzese wakimwimbia bwana wakati wa hafla hiyo

TAHA WALIVYOSHIRIKI MAONYESHO YA WAKULIMA (NANE NANE) MBEYA

Afisa kilimo Mkoa wa Mbeya (Aliyevaa tai) akipokea maelezo ya kilimo cha mboga ndani ya hema maalumu ya kuoteshea nyanya iliyowekwa na Barton Tanzania kwa ushirikiano na TAHAAfisa kilimo Mkoa wa Mbeya (Aliyevaa tai) akipokea maelezo ya kilimo cha mboga ndani ya hema maalumu ya kuoteshea nyanya iliyowekwa na Barton Tanzania kwa ushirikiano na TAHA  katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya
Afisa Kilimo na Msimamizi wa ofisi ya TAHA ukanda wa Nyanda za Juu Kusini Bw. Ringo (Mwenye Jaketi jekundu) akifafanua juu ya matumizi bora ya teknoloji za kisasa kwenye kilimo cha mboga ili kuongeza tija kwa MkulimaAfisa Kilimo na Msimamizi wa ofisi ya TAHA ukanda wa Nyanda za Juu Kusini Bw. Ringo (Mwenye Jaketi jekundu) akifafanua juu ya matumizi bora ya teknoloji za kisasa kwenye kilimo cha mboga ili kuongeza tija kwa Mkulima katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya
Mtaalamu wa Kilimo wa TAHA Bw. Anania Bansimbile akiwaonyesha wananchi namna bora ya kuotesha mimea ya mboga kabla ya kupandwa shambaniMtaalamu wa Kilimo wa TAHA Bw. Anania Bansimbile akiwaonyesha wananchi namna bora ya kuotesha mimea ya mboga kabla ya kupandwa shambani katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya
Chainizi iliyopandwa kwa ustadi wa hali ya juuChainizi iliyopandwa kwa ustadi wa hali ya juu
Hema maalumu(greenhouse) la kuoteshea mazao yanayohitaji joto ili yaweze kustawi vizuriHema maalumu(greenhouse) la kuoteshea mazao yanayohitaji joto ili yaweze kustawi vizuri
Plot ya TAHA na mshirika wake Barton kama inavyoonekana katika pichaPlot ya TAHA na mshirika wake Barton kama inavyoonekana katika picha
Mazao ya mboga yaliyopandwa kwa utaalamu wa hali ya juu kwenye vitalu vya mboga vya TAHAPlot ya TAHA na mshirika wake Barton kama inavyoonekana katika picha
Karoti iliyovunwa kutoka katika vitalu vya TAHA kwa ajili ya maonesho ya wakulima katika viwanja vya Nanenane MbeyaKaroti iliyovunwa kutoka katika vitalu vya TAHA kwa ajili ya maonesho ya wakulima katika viwanja vya Nanenane Mbeya
Wananchi wakipokea elimu kutoka kwa mtaalamu wa TAHA namna ya kuotesha nyanya kwenye hema maalumu ya kuoteshea mazao ya mbogaWananchi wakipewa elimu lishe kuhusu umuhimu wa matumizi ya mboga kutoka kwa mtaalamu wa masuala ya lishe wa TAHA Bi. Lawrencia wakati wa maonyesho ya Nanenane Mbeya
Mtaalamu akimuelekeza jambo Mkulima aliyetembelea Banda la TAHAMtaalamu akimuelekeza jambo Mkulima aliyetembelea Banda la TAHA

Sunday, March 9, 2014

Mnyate ‘Super Boy’ ‘Mtoto’ wa Kova aliyepania kufuata nyayo za Matumla

Na Michael Komba
NDONDI ni miongoni mwa michezo ambayo imewahi kuitangaza vilivyo Tanzania katika anga ya kimataifa, kama ilivyokuwa kwa riadha.

Mabondia ambao waliwahi kuipeperusha vyema Bendera ya Tanzania katika mashindano mbalimbali ya kimataifa, ni Michael Yombayomba, Habibu Kinyogori, Titus Simba, Emmanuel Mlundwa, Rashid Matumla na wengineo.

Soka ambayo ndio mchezo unaopendwa na kupewa kipaumbele zaidi hapa nchini, haujawahi kuiletea Tanzania mafanikio yoyote, zaidi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa Huru ya Afrika mwaka 1980 nchini Nigeria.

Zaidi ya mafanikio hayo, timu yetu ya Taifa, Taifa Stars na hata klabu zetu, zimebaki kuwa ‘kichwa cha mwendawazimu’ katika michuano mbalimbali ya kimataifa.

Angalau riadha na ndondi zimefurukuta kwa kutwaa medali katika mashindano makubwa kama michezo ya Olimpiki na Michezo ya Afrika (All Africa Games’.

Pamoja na hilo, mchezo wa ndondi bado unaonekana kupewa kisogo na wadau kwa kushindwa kuboresha miundombinu yake kama kumbu za kisasa na mengineyo kama hayo.

Hadi sasa, hakuna kumbi za kisasa za mchezo huo hapa nchini ambazo zingesaidia kuwahamasisha vijana wadogo wa kitanzania kujikita katika ndondi.

Hatahivyo, bado kila siku ya Mungu vijana wa kitanzania wameonekana ‘kupambana’ kujaribu kuendeleza vipaji vyao kupitia ndondi, baadhi yao wakifanya hivyo bila kupata uangalizi sahihi wa kitaalamu.

Mathalani, katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, unaweza kuwakuta vijana wadogo wakiwa wamening’iniza kiroba kilichojaa mchanga juu ya mti, wakijifua waweze kutimiza ndoto zao za kuwa mabondia maarufu hapa nchini na duniani kwa ujumla.

Wapo wanaofanya hivyo ili waweze kufikia mafanikio ya mabondia waliopita kama Yombayomba, Simba; lakini wengi wakisikika wakimtaja Rashid Matumla, ambaye ndiye bondia wa miaka ya hivi karibuni kuwahi kutamba hapa nchini na hata katika medani ya kimataifa, akitwaa mikanda lukuki kabla ya kustaafu.

Yusuph Mnyate ‘Super Boy’, ni miongoni mwa vijana wenye vipaji vya ndondi ambaye ameona ni vyema akakitendea haki kipaji chake hicho.

Kijana huyo mwenyeji wa mkoani Tanga, ni mwajiriwa wa Jeshi la Polisi chini ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akiwa anapatikana pale Polisi Ufundi, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam, ni miongoni mwa wachezaji wa timu ya ndondi ya Polisi jijini.

Na baada ya kudumu katika ndondi za ridhaa kwa muda mrefu kidogo, Mnyate ameamua kubadili upepo na kuhamia kwenye ndondi za kulipwa.
Akizungumzia uamuzi wake wa kuhamia ndondi za kulipwa, Mnyate anasema kuwa alifanya hivyo kama sehemu ya hatua za maisha yake katika mchezo huo aliodai kuwa anaupenda mno.

“Nimekuwa katika ngumi za ridhaa kwa muda mrefu, na sasa nimeamua kuhamia ndondi za kulipwa, nikiamini ninaweza kupata mafanikio makubwa kwani nina usongo wa kulipa sifa Jeshi la Polisi pamoja na nchi yangu kwa kufanya mambo makubwa kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa.

“Katika maisha yangu ya ndondi, nimekuwa nikipata sapoti ya hali ya juu kutoka kwa mwajiri wangu na wachezaji wenzangu ambao nao ni askari Polisi… naondoka ngumi za ridhaa kwenda za kulipwa, nataka kurejesha hadhi ya ndondi ndani ya Jeshi la Polisi.
“Matarajio yangu ni kufuata nyayo za Haji Matumla ambaye ni askari Polisi, Yombayomba (Michael) na wenginbeo, ikiwezekana hata kuwazidi, naamini hilo linawezekana kama kila kitu kitakwenda kama nilivyopanga.”
Aliongeza: “Nataka kufanya kitu tofauti, nashukuru hata rafiki na ndugu zangu, wananisapoti, sitaki kubahatisha, ndio maana nimetafuta kocha mzuri mwenye uzoefu, kama Rashind Matumla, ambaye nashukuru amenipokea na kunikaribisha katika ‘gym’ yake.
“Kwangu Rashid Matumla ni mtu muhimu sana, nimekuwa nikimshabikia tangu nilipokuwa mtoto na nilitamani siku moja nije kuwa kama yeye au hata kumzidi.
“Kufanya mazoezi katika ‘gym’ yake (Matumla), kunanisisimua sana, ninapoona picha zilizopo katika ukuta wa gym yake akiwa anapigana, akiwa amebeba mikanda mbalimbali ya ubingwa wa Dunia, na hata habari za kwenye magazeti za kumpongeza, ninapata hisia kali sana.”

Anasema kuwa kikubwa zaidi, ni kuona bingwa huyo wa zamani wa Dunia wa WBU ambaye alishiriki mara tatu michezo ya Olimpiki, mwaka 1988, 1992 na 1996, akimpa moyo wa kufuata nyayo zake 

“Kaka Rashid amekuwa akinipa moyo kuwa kutokana na jinsi alivyoniona, ninaweza kuwa bondia mzuri kama yeye au hata kumzidi, lakini kama nitafanya bidii katika mazoezi, kuzingatia nidhamu na miiko ya mchezo huu wa ngumi.”

Mnyate anaelezea hali ya ndondi ilivyo ndani ya Jeshi la Polisi, akisema: “Polisi kuna wachezaji wazuri sana, tatizo ni hamasa, hivyo nimeona ni vyema nikawafungulia njia wenzangu kwani hakuna sababu yoyote ya kutofika mbali katika mchezo huo, maana mwajiri wetu anajali sana michezo si kama katika sekta nyingine.”

Kwa upande wa ndondi za ridhaa, anasema kuwa tatizo lililoko huko ni uongozi wa chama husika kutokuwa na mikakati ya kuuendeleza mchezo huo.

“Katika ngumi za ridhaa hapa nchini, tatizo ni uongozi, pale kuna mtu mmoja tu, Mashaga (Makore), jamaa anajitahidi sana kupambana, kama angepata msaada, basi mambo yangekuwa mazuri zaidi,” anasema.

Na sasa Mnyate ni ‘hakuna kulala’, kila baada ya kumaliza majukumu yake ya kikazi, hugeukia mazoezi ya ndondi katika gym ya Matumla na wakati mwingine kwenda kwenye klabu nyingine za mazoezi.

Katika mazoezi yake hayo, wakati fulani amekuwa pia akinolewa na Haruna Andrew ‘Ndimu Mkata Shombo’ ambaye naye ni bondia.

Matarajio yake kwa siku chache zijazo ni kupata pambano la kujipima nguvu dhidi ya bondia atakayejitokeza kukabiliana naye.

“Kabla ya kupata pambano, niliona ni vyema nikajifua kwanza kwani kuna kipindi nilisimama kufanya mazoezi, hivyo lazima niwe fiti kabla ya kupanda ulingoni,” anasema.

Anasema kuwa matarajio yake mapema mwezi ujao atakuwa fiti tayari kuonyesha ubabe na bondia yeyote atakayekubali kupigana naye.

Hata hivyo, alisema kuwa katika kufanikisha azma yake hiyo, hatasita kuwa bega kwa bega na mwajiri wake ambaye ni Jeshi la Polisi kuhakikisha kipaji chake hicho hakiathiri majukumu yake ambayo ndiyo yanayomwezesha kufanikisha baadai ya mambo kuelekea mkakati wake wa kuwa bondia hatari hapa nchini.

“Pamoja na haya yote, ninaiheshimu sana kazi yangu kwani ndiyo inayonifanya niwe na jeuri ya kutamba kutaka kufuata nyayo za akina Matumla, bila Jeshi la Polisi, nisingekuwa kama nilivyo sasa,” anasema Mnyate.

Bondia Yusuph Mnyate, alizaliwa Februari 20, mwaka 1982 katika eneo la Ngamiani, jijini Tanga, akiwa ni mtoto w asaba katika familia ya watoto saba wa Mzee Mnyate.

Alianza masomo yake katika Shule ya Msambweni, jijini humo na baadaye kujiunga na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) mwaka 1995.

Mnyate ambaye kwa sasa hajaona, lakini akiwa na mchumba anayetarajia kufunga naye ndoa muda si mrefu, alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 2000 na hadi sasa analitumikia jeshi hilo, kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.
Pamoja na kulitumikia Jeshi la Polisi na kuendeleza kipoaji chake cha ndondi, Mnyate anekuwa akitenga muda wake kwa ajilki ya kujiendeleza kimasomo.

“Kama unavyofahamu, elimu ni kila kitu na haina mwisho, nashukuru mwajiri wangu (Jeshi la Polisi), hana kikwazo na mtu anayetaka kujiendeleza kimasomo, kwa kweli ninashukuru sana kwa hilo,” anasema Mnyate.

Juu ya mkakati wake wa kuendelea na masomo, anasema: “Ndondi inaonekana kama ni mchezo wa akina ‘Kayumba’ (watu wasio wasomi), tusikubali ujinga, mabondia twendeni shule.”

Kuhusiana na malengo yake baada ya kuanza kupata mafanikio katika ndondi, anasema amepania kufungua klabu yake ya mazoezi ya ndondi (gym) ambayo itakuwa katika ubora wa hali ya juu ili kuwawezesha vijana chipukizi kujinoa waweze kutimiza ndoto zao.

“Lengo langu ni kufungua ‘gym’ ambayo itakuwa na hadhi ya kimataifa, kama ilivyo Azam Complex ya klabu ya soka ya Azam.

Juu ya kilio cha mabondia wengi kutaka wadhamini kujitokeza katika mchezo huo, Mnyate anaasa: “Tusitegemee zaidi wadhamini, tujitegemee, tusipigane kuganga njaa, kwani tunadhalilishwa kwa kutojitambua, maana ukipigwa unajirudisha nyuma na umaarufu wako unapotea.”

MSETO tunamtakia kila la kheri Yusuph Mnyate kuelekea jitihada zake za kuwa bondia wa kulipwa mwenye mafanikio hapa nchini, tukiamini hilo linawezekana iwapo atajipanga hasa na kuzingatia miiko ya mchezo huo.

Kwa maoni, ushauri 0783324232